muhosni
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 1,108
- 154
8.1.6 Kutokuwepo Mwongozo Unaoelekeza Maagizo ya Wizara Yanayotakiwa Kutolewa kwa Mashirika
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ni shirika huru ambalo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge yaani Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania, CAP 364 ya mwaka 1962 na kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 1992. Jukumu kubwa la msingi likiwa ni kutangaza na kuendeleza utalii Tanzania. Shirika hili likiwa shirika huru, lina mamlaka ya kujiendesha lenyewe chini ya usimamizi na maelekezo ya Bodi ya Wakurugenzi bila kuingiliwa. Nimebaini kuwepo kwa shughuli zinazoashiria Wizara ya Mali Asili na Utalii kuingilia utendaji wa shughuli za Bodi ya Utalii. Kwa mfano Wizara ilihamisha jumla ya Shilingi milioni 771.2 (2011: Shilingi Milioni 591) kwenda Bodi ya Utalii kwa shughuli ambazo siyo za Bodi ya Utalii. Fedha hizi zilichukuliwa tena na kurudishwa Wizarani kwa maagizo ya Wizara. Jambo la kushangaza zaidi ni pale ambapo jumla ya Shilingi milioni 416.1 zilichukuliwa kutoka Bodi ya Utalii na mfanyakazi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii na Shilingi milioni 355.096 zililipwa moja kwa moja kwa idara nyingine au watoa huduma wengine kama Wizara ilivyoelekeza. Muingiliano kama huu katika shughuli za kiutendaji unakwamisha uwajibikaji katika shughuli za Bodi ya Utalii.
Wizara ya Mali Asili na Utalii pia, ilitoa maagizo mbalimbali ili yatekelezwe na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Baadhi ya maagizo ya kiutekelezaji yaliyotolewa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni: Kutoa mchango wa Shilingi milioni 34.96 kwa Wizara ya Mali Asili na Utalii ikiwa ni kwa ajili ya mshahara wa miezi minne (4) wa Afisa Utalii ambaye kituo chake cha kazi ni Japan, Ngorongoro kulipa gharama za wabunge walioshiriki maonyesho ya utalii ya kimataifa. Zaidi ya hapo, Wizara ilielekeza kuwa Mbunge mmoja awe akilipiwa gharama za kuhudhuria maonyesho kama hayo kwa siku za mbele japo uongozi wa Ngorongoro haukuafiki jambo hilo. Ngorongoro ilielekezwa na Wizara kulipa Shilingi milioni 340 kwa ajili ya kutangaza utalii huko Marekani, kulipia gharama za watu watatu (wajumbe wawili wa Bodi na mfanyakazi mmoja) kuhudhuria mkutano wa kamataifa kwa ajili ya mafunzo ya kurejesha na kutunza vitu vya kiutamaduni ambao ulifanyika Roma kuanzia tarehe 14-16 Novemba, 2011. Pia, Wizara ilitoa maagizo ya kuchanga Shilingi bilioni 5.171 kwa ajili ya gharama ya kununua helicopter aina ya Bell 407 japokuwa agizo hili halikutekelezwa. Bodi katika kikao chake cha 101 tarehe 27 Oktoba, 2011 iliridhia na kuelekeza kuwa maagizo yote ya wizara yatekelezwe
Imenukuliwa kutoka report ya CAG ya mashirika ya umma