Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad (kulia) baada ya kumwapisha Ikulu Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal
.
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Profesa Mussa Assad amesema ataanza kazi kwa moto uleule ulioachwa na mtangulizi wake, Ludovick Utouh aliyestaafu.
Akizungumza jana mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Profesa Assad aliyeteuliwa Novemba 5 kushika wadhifa huo alisema: Ninasubiri niingie ofisini nianze kazi
nitaendeleza yote yaliyoachwa na mwenzangu, sitatoka nje ya mstari.
Profesa Assad alisema yuko tayari kusimamia utendaji kazi wa kisasa kwa kusimamia misingi ya ofisi yake, ili kulinda hadhi na heshima aliyopewa na Rais katika uteuzi huo.
Kuhusu Ripoti ya Akaunti ya Escrow, Profesa Asaad alisema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa hiyo na maagizo yote yaliyotolewa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyopo chini ya ofisi yake na kuendeleza yale ambayo yalishaanza kutekelezwa.
Alisema moja ya mambo ambayo atayafanyia tathmini na kupatia majibu ni kutotajwa moja kwa moja katika Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kama fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa pamoja na Tanesco na IPTL ni za umma au vinginevyo.
Utoh anena
Akizungumza katika hafla hiyo, Utouh alisema kuwa amemkabidhi Profesa Asaad ofisi yenye watendaji wanaofanya kazi kwa ari na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.Alisema amefurahishwa na uteuzi wake na kusema anaamini ataendeleza uwajibikaji na umadhubuti wa ofisi hiyo kwa manufaa ya Taifa.
Utouh alimkabidhi Profesa Asaad mwongozo maalumu wenye kurasa 78 na kueleza kwamba utampa mwelekeo wa namna ofisi hiyo ilivyo na iwapo kuna upungufu yuko tayari kutoa ushirikiano.
Spika Makinda
Akimzungumzia Profesa Asaad, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema mtikisiko uliolikumba Taifa kutokana na Kashfa ya Escrow umelifanya lijenge misingi mizuri zaidi ya kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.
Alisema anaamini CAG mpya ataingia na mfumo wa kisasa zaidi na kusaidia kuweka miundo bora zaidi ya kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia mapato na matumizi ya Serikali.
Chanzo: Mwananchi
Hapa hamna kitu ni mambo yale yale tu. Bora hata Uhouh alikuwa kwa kiasi kurevieal mambo akijiamini na akafanikiwa.
Hamna Professor aliyefanya vyema katika nafasi hizi za kuteuliwa a chilia mbali za kuchagua. wote wameprove failure, wachumia tumbo waoga, wasio na maamuzi, wasio na maono na wavivu kiutendaji. Mifano michache ni hii
1. Professor Jumanne Maghembe na domo lake la kusema by anavyochemsha wizara ya maji! Mnbali na misaada na mikopo serikali imepata kwa sector ya maji bado mchwa wa CCM wako wanatafura professor anapiga domo tu bila kuleta mipango sanisfu ya kumaliza tatizo la maji mijini na vijijini. uwezo mdogo wa kushauri serikali na kusimamia funds za maji zifanye kaze husika.
2. Professor Benno Ndulu! Mipango mibovu ya kifedha kwa Tanzania, mfumuko wa bay, High interest rates kwa mabank , fedha haram na utatishaji wake e.g. FBME. Matumizi ya US dolla Tanzania kwa huduma zinazotolewa Tanzania. Fedha nyingi feki kwenye mzunguko, Noti dhaifu sana za bongo, cash kuhamishwiwa nje kupitia bank zetu nas mengineyo mengi.
3. Professor Mark mwandosya nadani mnafahamu na mnamuona wenyewe utumbo anaooungea publically. Kama vile hakwenda shule. Anabaki tu akitetea mabo ya kijinga mpaka inakuwa kero kwa jamii.
4. Professor Muhongo nadhanai mmemsikia wenyewe na dahrau zake na kijeli kwa Tanzania. Nakumbuka alivyotaka kujilinda wakati wa bunge la budget kwa kutumia gossips kumnyamazisha Ole sendeka baada ya kusema itabidi tuite CV za wabunge wengine kwani kuna waliopata zero form six akimmaanisha O..S. kama professor haya manaeneo sio!!
5. Professor Shivji alivyoanza kutetea Katiba ya CCM na serikali mbili na kusahao aliyokwisha kuyaandika ni dhihaka ya maprof wetu.
6. Professor Mkulo alivyockemsha wizara ya Fedha
7. Professor Anna tibaijuka na failure kwenye ardhi na makazi
8. Professor Mosolla ndio kabisaa mpaka anafika mahali akabaki na kaubunge tu.
9. Na kwa sasa Professor JK wa Kichina kwenye kilimo!!
Hawa ni baadhi tu muone jinsi maprofessor walivyo na utendaji mbovu. waachwe kwenye taasisi za elimu na sio kwenye huduma muhimu zinazohitaji wawajibikaji.
'Nawasilisha