CAG abaini ufujaji wa fedha serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG abaini ufujaji wa fedha serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 10, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habel Chidawali,Dodoma
  MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovick Utouh amesema serikali inafanya mambo bila mpangilio katika matumizi yake pamoja na kuanzisha mamlaka bila ya kuwa na mipango kamili.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema amebaini madudu makubwa kwa Wilaya za Kishapu, Rombo na Kilosa ambako sehemu zote zinaonekana fedha nyingi zimetumika bila ya mipango.

  Mbali na maeneo hayo, Utouh alibainisha eneo jingine la matengenezo ya magari ya serikali ambako, alisema hakuna mipango mahususi ya jinsi ya kusimamia fedha za walipakodi.
  Utouh alitoa kauli hiyo katika viwanja vya bunge alipokuwa akizungumzia kuhusu ripoti tano alizoziwasilisha jana bungeni, kuhusu ukaguzi alioufanya katika maeneo mbalimbali nchini.

  “Kikubwa nilichobaini ni kwamba, serikali imekuwa ikifanya mambo mengi bila ya mipango madhubuti ikiwa ni pamoja na kuanzisha mamlaka hata bila ya kuwa na maandalizi jambo ambalo ni hatari,’’ alisema Utouh.

  CAG alitolewa mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kuwa ilianzishwa pasipokuwa na mipango maalumu, katika maandalizi ya kuanzishwa kwake jambo lililosababisha serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh6.7 bilioni kwa kipindi cha miaka mitatu tu.

  Mbali hilo,alisikitishwa na jinsi ambavyo serikali inashindwa kujipanga katika kuwadhibiti watumishi wake kwani katika kipindi cha miaka minne Kishapu imekuwa na wakurugenzi wanne na waweka hazina wanne pia.

  Alisema alitumia nafasi yake aliyopewa kwa mujibu wa katiba, kukagua wilaya ya Kishapu kama mfano wa maeneo mengine ambayo yamekuwa na matatizo yanayofanana na hayo.

  Akizungumzia suala na ubadhirifu wa fedha katika matengenezo ya magari ya serikali kiongozi huyo alisema, “lile ni tatizo la nchi maana magari yaliyopo ni mengi na gharama za matengenezo wakati mwingine zinazidi hata gharama za manunuzi.’’

  Alisema serikali kupitia Wizara ya Ujenzi haina mipango mizuri wala mwongozo wa matengenezo ya magari yake na kwamba, wamebaini wakati mwingine serikali inalipa fedha hata kama matengenezo hayakufanyika.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mitaa, Agustino Mrema aliilaumu serikali kuwa imekuwa ikipuuza mara nyingi ripoti za CAG na hivyo hata kama angekuwa na mapendekezo mazuri hayafanyiwi kazi.

  Mrema alishutumu serikali kuwa imekuwa ikiwalinda kwa kiasi kikubwa watuhumiwa wa ufujaji wa fedha za serikali kutokana na wakati mwingine inafanya kazi ya kuwahamisha wezi hao.
  “Serikali kuna mtandao tena ni mkubwa, maana watu wanahamisha wizi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, lakini pia ushauri wa CAG huwa haufanyiwi kazi kabisa,’’ alisema Mrema.

  :A S 465:
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  this man still has the guts to stand and fumble publicly? Or may b he is trying to divert public attention from docs issue!
   
Loading...