Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya droo ya makundi ya kutafuta nafasi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 ambapo machuano hiyo itafanyika nchini Cameroon.
Kufanyika kwa droo hiyo kumekuwa ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuanza kwa Kombe la Mataifa Afrika ambalo linafanyika nchini Gabon.
Makundi ambayo yametangazwa ni kumi na mbili, kila kundi likiwa na timu nne na Tanzania ikiwa kundi L ambalo lina timu za Cape Verde, Uganda na Lesotho.
Michezo ya makundi inataraji kupigwa kuanzia mwezi Juni na kumalizika Novemba, 2018.
Chanzo: Mo Blog
=======
Habari hii imetumika ktk JamiiLeo