CAF yaiondoa ES SETIF Ligi ya Mabingwa!!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limetangaza kuindoa ES Setif ya Algeria katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Caf imetangaza kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kuwa Setif wameondolewa baada ya mashabiki wao kufanya vurugu katika mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns maarufu kama Masandawana.
Mashabiki hao walianzisha vurugu kubwa na kusababisha mchezo huo kusimama kwa kipindi kirefu, baadaye mwamuzi akalazimika kumaliza mpira wakati mashabiki walipoamua kurusha mawe, chupa na vitu vingine uwanjani wakionyesha kutofurahishwa kwa kuwa timu yao ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0.

Huenda hilo linaweza kuwa funzo kwa mashabiki wa soka nchini hasa wale wa Yanga ambao timu yao inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, kwamba hawatakiwi kufanya vitendo vya kihuni kwa kuwa Caf, hawana mchezo katika hilo.

Katika hatua ya makundi ES Setif ilikuwa ikitane na Zamalek katika mechi yake ya pili iliyopangwa kupigwa Juni 29 jijini Cairo, Misri lakini sasa safari imewakuta.
 
Waarabu ndio wafanya fujo maarufu ,acha wapate haki yao.Na haya mafataki uwanjani mpaka mpira unasimama yasiruhusiwe na CAF
 
Hivi kipindi kile ma fans wa zamalek wanamrushia juma kaseja mkojo mbona awakutoa comment!
 
Hawa yeboyebo si wanajifanya manunda kutulingia kila siku eti wakimataifa, sasa na sisi tutawaonesha kuwa ni watoto wa mjini kitambo, unapiga uzi wa yeboyebo unaanzisha varangati la uongo na kweli ili CAF wapate kaclip ka kuwadelete watu afu tukutane mchangani. Tuone sasa hizo ndege mtapandia wapi!!!!!!! Hahahahahhahhaha siko serious sana.
 
Ikitokea hii ntafurahi mno .....sipendi Yanga kama nini
 
Wamewaonea tu..mbona urussi hawakutolewa, CAF inajifanya ipo makini kumbe hawana lolote.
 
Hawa yeboyebo si wanajifanya manunda kutulingia kila siku eti wakimataifa, sasa na sisi tutawaonesha kuwa ni watoto wa mjini kitambo, unapiga uzi wa yeboyebo unaanzisha varangati la uongo na kweli ili CAF wapate kaclip ka kuwadelete watu afu tukutane mchangani. Tuone sasa hizo ndege mtapandia wapi!!!!!!! Hahahahahhahhaha siko serious sana.
Tupo pamoja mi nitajitolea kununua yale mafataki,zile nyondo za Jerry Murro Nadhani hii ndio dawa yake,naanza kufanya maandalizi sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom