wakuu nina swali ambalo kila muda linaniumiza kwenye maswala ya mpira
hivi ni kwanini katika klabu bingwa Africa team za kiarabu zinamaliziaga mechi zao nyumbani unless zikutane zenyewe kwa zenyewe tu au ni kwa sababu makao makuu yapo arabuni
cha muhimu timu zetu zipambane bila ya kujali wanaanzia wapi na kumalizia wapi hapo tutafanikiwa lakini tukitegemea hili swala la kusema sisi kila siku tunafanyiwa hujumu tunapo kwenda huko litafanya tuwaogope na hatuta fanikiwa tukiwa na hofu.
uzuri ni kwamba kama ni hujuma tumefanyiwa mara nyingi hivyo nilitegemea timu zetu zitafute njia za kutatua hayo matatizo binafsi bila kuwategemea CAF kwani naamini timu bora haichagui nyumbani au ugenini ubora wake uta kua palepale
shukran!.....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.