CAF Confederation Cup Aazam yarushwa hadi round ya kwanza

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
230
250
Draw iliyofanyika Misri Leo inaonyesha Kuwa AZAM FC wana Lambalamba ni moja kati ya timu 12 Zitakazoanzia Round ya Kwanza ya Michuano ya CAF Confedaration Cup 2017. Timu zingine 40 zitaanzia na stage ya Mtoano (preliminary stage)

Azam itacheza Mechi ya Kwanza Tarehe 10–12 March 2017 na mshindi wa Mechi ya awali namba 12 kati ya Orapa United(Botswana) VS Mbabane Swallows(Swaziland)

CAF kuelekea michuano ya mwakani imebadilisha mfumo wa mashindano hayo, ambapo imepanua wigo kwa timu zitakazoingia hatua ya makundi kutoka nane hadi 16, kila michuano itahusisha makundi manne yenye timu nne kila moja.

Mfumo huo unamaanisha kuwa timu 32 zitakazocheza raundi ya kwanza inayofuata baada ya ile ya awali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, zile 16 bora zitakazoshinda zitaingia moja kwa moja katika hatua ya mwisho ya mtoano (play off).

Katika hatua hiyo zitakutanishwa na timu nyingine 16 zilizotolewa katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na wale 16 bora watakaopenya hapo watafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi, itakayoanza kuchezwa Mei mwakani.
 

Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,408
2,000
Azam mara hii nao wakaze sio kuwakilisha tu.Hivi simba iliwakosea nini? Yaani bila kutaja simba mtu anaona hajazungumza mpira wa bongo.
 

Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Wanawake wakiwa saloon si huwa wanazungumzia wanaume wao.Usiwashangae mashabiki wa migongo wazi ni lazima wamtaje mume wao.
 

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,407
2,000
Azam mara hii nao wakaze sio kuwakilisha tu.Hivi simba iliwakosea nini? Yaani bila kutaja simba mtu anaona hajazungumza mpira wa bongo.
Usikasirike Mkuu...

Ndio utani wa Jadi huo!....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom