MATUTA BARABARANI KUTOZINGATIA UTAALAM
Hivi karibuni, kumezuka mtindi wa wananchi kujiwekea matuta ya barabarani (road bumps) kwa kienyeji bila kufuata utaratibu wa kitaalam. Hii katika barabara za vumbi au changarawe. Matuta haya yamekuwa na athari chanya nyinginkwa watu na vyombo vya usafiri,hasa magari. Yanarefushwa sana kwenda juu, lakini yakiwa na upana mdogo sana kiasi kwamba, magari, hasa yale madogo madogo yanapita kwa taabu sana, ama kushindwa kabisa kipita mpaka lipate msaada wa kusukumwa.
Cha ajabu, mamlaka zinazohusika (Tanroads na TARURA) wako kimya tu bila kujali madhara yanayosababishwa na matuta haya kwa magari na watu pia.
Sipingi haja ya kuwa na matuta haya. Ila, mamlaka zingesimamia wananchi waweke kwa kufuata utaalam usionna athari kwa watu na vyombo vya usafiri.
Ukurasa hautishi,vinginevyo ningeorodhesha madhara au athari hizi kwa undani.
Mwisho, naomba mamlaka zisimamie ili yalokwisha kuwekwa yafumuliwe na kuwekwa mengine kitaalam.