Kabla ya tukio hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo alibadilishwa hiyo ilikuwa ni miezi 3 iliyopita ndipo walipoanza kupata vipeperushi vya vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana wakitishia kuuwa walimu na kuchoma shule ndipo jana hiyo usiku shuguli hiyo ikatendeka ,haieleweki haswa kisa ni kuhamishwa yule mwalimu au kulikuwa kuna matatizo mengine zaidi shuleni hapo
leo hii asubuhi ndugu na wazazi wengi wa wanafunzi wale wamefika shuleni hapo pamoja na wanafunzi huku mtiani wa mock kwa kidato cha 6 ukiwa unaendelea naamini vyombo husika watapatia jawabu lake na kuieleza jamii nini haswa kinaendelea katika shule ile .
Ikumbukwe pia pale kulikuwa na mradi wa ict huu mradi haijulikani umeishia wapi na mafanikio yake yalikuwa ni nini kwa wakazi wa kijiji hicho na tanzania kwa ujumla mradi huo umekufa kimya kimya