DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Seleman Bungara maarufu "Bwege" amemtaka Rais Samia kutoa majibu kuhusu tuhuma zinazohusu kutekwa kwa baadhi ya watu, Bwege amesisitiza kuwa kukaa kimya katika tuhuma hizo ni sawa na kuthibitisha ukweli wake. Amesema kuwa kama Rais atatoa majibu, wananchi wataweza kuyapima maneno yake dhidi ya matukio yanayofanyika.
Aidha, Bwege alidai kuwa kama serikali inge kuwa na dhamira ya kubaini wahusika, haingeshindwa, kwani kikosi kinachohusika kinajumuisha mchanganyiko wa polisi, watu wa usalama, na wanajeshi, kinachoitwa “Task Force.”
"Kama kweli serikali ingekuwa inataka kuwa shughulikia watu ambao wanafanya hayo wasingeshindwa kuwajua na kuwakamata na sisi wengine tunaamini wanawajua na hicho kikosi mimi mwenyewe najua mimi nikiwa mbunge niliambiwa na mtu mkubwa sana kuna kikosi kinaitwa task force ambacho kina mchanganyiko wa polisi, usalama na wanajeshi ambao wameondolewa katika kikosi hicho" Seleman Bungura (Bwege) Akizungumza na Mwanahalisi Tv