Bwana Rwegoshora

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,607
Reaction score
167,399
Baada ya kumaliza degree yake ya sheria mlimani Bwana Rwegoshora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya kuhudumia clients(wateja) .

Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake.Hapo ndipo alipoanza kunyanyua mkono wa simu ya TTCL,wakati anajizungusha kwenye viti virefu.
Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha wakati anaongea na simu,alisikika akiongea
'' No.no, no, Absolutely no, You tell those clowns in New York that I won't settle this case for less than one million. (pause)
Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next week,
I'll be handling the primary argument and the other members of my team will provide support. Okay..
Pliz dont forget to tell the State Prosecutor that I'll meet with
him next week to discuss the details."
Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga kwa muda zaidi dakika 5.
Baada ya kumaliza kuongea na simu,bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa.


''Samahani sana , kwa kukupotezea muda wako, unajua tena kazi zetu hizi unaumiza kichwa sana ,kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani niko busy sana ,ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe.
enh by the way, what can i do for you?
Jamaa alijibu.
'' Mimi ni mfanyakazi wa TTCL,nimekuja kuunganisha line yako ya simu''.

(Bwana Rwegoshora kaishiwa nguvu)
Palikua padogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…