Bwana harusi mtarajiwa hajatokea kwenye sendoff

Bwana harusi mtarajiwa hajatokea kwenye sendoff

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
4,322
Reaction score
6,700
Wakuu hii imekaaje,sitosema nilipo maana inawezekana mhusika akawa humu,

Kisa ni kwamba kuna dada mmoja wa kitaa,huwaga ananata sana kama super glue,naye yamemkuta,kuna mwana alimuotea akaahidi kumuoa,akafuata taratibu zote kuelekea kwenye ndoa,ila siku ya sendoff mwana hakutokea,ikawa aibu kubwa kwa huyu mwanamke na familia yake,hivi mkasa kama huu umewahi kutokea kweli somewhere?sasa hivi huyu mwanamke amekuwa cha wote,

Mdada aliyekuwa anajifanya yupo makini na mambo yake ya maisha,kaja kuumbuliwa na mhuni tu,mtaani minong`ono haiishi na maneno ya kumlaani kuwa atakula jeuri yake,leo nimemuona nikakumbuka kulileta tulijadili na kupeana uzoefu kwa waliowahi kukutana au kuusikia mkasa wa namna hii,

Mimi nimeshangaa sana na kumhurumia huyu mwanamke traffic officer!
 
Alimuamini kupita kiasi, hata kwenye ndoa usiamini kila kitu kwa kiasi kikubwa...

There is only one truly faithful friend for any man or woman – the Lord Himself! He is a very present help in trouble. “It is better to trust in the LORD than to put confidence in man” (Ps 118:8).
#supernaturalincrease
 
Kwani taratibu za harusi zinaendeleje au zimesitishwa
 
Inategemea na imani ya wahusuki
Kwa Muslim hauwezi kuhudhuria sherehe ya kuagwa mwanamke yeye haimuhusu kabisaa
Hapo labda kama muda wa ndoa umepita ndio wapate wasiwasi
 
una hakika sio kajificha ili bibi harusi mtarajiwa apate taaaaabu kumtafuta?
 
Back
Top Bottom