BVR: Uwezekano wa kujiandikisha zaidi ya mara moja

mzeemzima

Senior Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
132
Reaction score
87
Naomba kujuzwa wakuu, hivi haiwezekani mtu akajiadikisha zaidi ya mara moja kwa mfumo huu wa BVR?

Mategemeo yangu ilikuwa ni kwamba data zote za usajili kwa kuwa ziko katika electronic format ziwe katika central database ambayo ingekuwa inakuwa queried na kila wakala kucheki kwanza kama mtu anayetaka kujiandikisha tayari ameshaandikishwa au la, kwa kuagalia finger prints ambazo zinachukuliwa wakati wakati wa kujiandikisha, lakini sijaona kitu kama hicho kikifanyika.

Lakini kingine ambacho sijaona kikifanyika ni verification ya kujua kama huyu mtu ni raia au la naona kila mtu anayekwenda kituoni anaandikishwa tu.

Sasa kwa haya yote hatuoni kuwa kuna uwezekano wa watu kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuweza kupiga kura zaidi ya mara moja?
 
mimi nimeshuhudia watu kadhaa wameandikishwa bila hata kutia finger prints, mashine ikishindwa kuscan alama za vidole wakala anakuuliza kama tayari kuchukua ivyo ivyo na ukikubari anakupa, kwa hiyo kwa tyle hii inawezekana kabisa mtu kujiandikisha mara mbili!

Sasa hili si ndio bao la mkono lenyewe? Kwa sababu hebu fikiria kwa mfano watu 10,000 kwa makusudi kabisa wakajiandikisha mara 10 au zaidi sehemu mbalimbali za Dar es salaam pekee ? halafu siku ya kupiga kura wanazungukia sehemu zote na kupiga kura, inamaanisha wataongeza kura 100,000 kwa huyo wanayemtaka wao. Najua wengie watasema ukipiga kura unapaka wino lakini ukweli ni kuwa ule wino ni rahisi sana kuufuta na kuhamia kituo kingine na kupiga tena kura kama ulijiandikisha sehemu tofauti tofauti . Na kumbuka kuwa hii inaweza kufanyika nchi nzima.
 
Zoezi limeenda kiujanja ujanja sana...ila ndio mambo yanavyokwendaga kwenye hii nchi
 
Sio rahisi kwa mashine hizo mtu kujiandikisha mara mbili iwapo amechukuliwa finger print hata kama data hizo hazijaenda central database.Nilikuwa mwandikishaji na siku moja mtu mmoja alikuja kuandikisha kwangu bahati mbaya nilijaribu mara mbili mashine ikawa inadetect kajiandikisha,nilipomuuliza akaeleza kuwa ukweli,na hapo ilikuwa hata majina niliyoandika yalikuwa hayajapelekwa central database kwa kutumia flash wala online.

Itadetect iwapo mara zote amechukuliwa fingerprint vinginevyo haita-detect
 
Uwezekano upo kama atajiandikisha vituo tofauti lakini mwisho wa siku data zote zinaunganiswa ndipo duplicate zitajulikana na wa naweza kuwa fungua mashitaka au kuwafutia sifa na nk kulingana na sharia za tume
 
Kuna waya flani Hivi na kiantena kwenye bvr kimeandikwa GPS sijui kina fanya kazi gani.
 
Ule waya ni GPS ambayo inaonyesha machine ipo eneo gani,saa ngapi imewashwa na saa ngapi imezimwa pia kama kuna uwezekano wa kutuma data online kile kinahusika.
 
Ile ni kama komputa yenye internet ukishaingiza data tayari zinakuwa kwenye central database kwa hiyo ukigonga dole gumba popote duniani kwenye mashine ya BVR inaonyesha
 
Yap kitakuwa kinatuma data Kuna kipindi muandikishaji alisitisha kuandikisha akawa anakirekebisha kwa kukiamisha amisha ku search network.
 
kuhusu kujiandikisha mara mbili inatakiwa isiwezekane maana once fingerprints zako zikiwa kwenye system ukija kuweka tena vidole pale inaonyesha hapohapo kwamba wewe upo kwenye system ya BVR tayari.
Ila swala la kuverify kama wewe ni raia, hili haliangaliwi kabiiisa kwa kwa kweli, na uwezekano wa mtu ambaye sio raia kujiandikisha upo kwa asilimia mia moja. Na pia hata vile vitambulisho vya zamani vya kupigia kura hawatilii maanani kuviulizia au kuvichukua kwa hiyo watu wengine wamebaki navyo, na ninavyofahamu mifumo ya hii nchi yetu hivyo vitambulisho vya zamani vinaweza kuendelea kutumika the way they see fit.
Yani ni ajabu sana kwa kweli watu wanaruhusu kwenda kujiandikisha bila aina yoyote ya kitambulisho cha kukutambua. Maswali yenyewe yanayoulizwa ni machache tu kiasi kwamba hata kama hujui kiswahili unayakariri tu.
 
Yap kitakuwa kinatuma data Kuna kipindi muandikishaji alisitisha kuandikisha akawa anakirekebisha kwa kukiamisha amisha ku search network.

ile ni gps antena kazi yake ni kuonyesha location ya bvr ilipo tu haina kazi nyengine
 
Naomba kujuzwa wakuu, hivi haiwezekani mtu akajiadikisha zaidi ya mara moja kwa mfumo huu wa BVR?

Mategemeo yangu ilikuwa ni kwamba data zote za usajili kwa kuwa ziko katika electronic format ziwe katika central database ambayo ingekuwa inakuwa queried na kila wakala kucheki kwanza kama mtu anayetaka kujiandikisha tayari ameshaandikishwa au la, kwa kuagalia finger prints ambazo zinachukuliwa wakati wakati wa kujiandikisha, lakini sijaona kitu kama hicho kikifanyika.

Lakini kingine ambacho sijaona kikifanyika ni verification ya kujua kama huyu mtu ni raia au la naona kila mtu anayekwenda kituoni anaandikishwa tu.

Sasa kwa haya yote hatuoni kuwa kuna uwezekano wa watu kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuweza kupiga kura zaidi ya mara moja?
Nina uhakika kabisa tena bila shaka watu wanajiandikisha mara mbili especially wanafunz wa IFM,CBE,DIT,TIA.najiuliza kwannn system ina accept hayo
 
Uwezekano upo kama atajiandikisha vituo tofauti lakini mwisho wa siku data zote zinaunganiswa ndipo duplicate zitajulikana na wa naweza kuwa fungua mashitaka au kuwafutia sifa na nk kulingana na sharia za tume

upo sahihi kabisa zoezi la kujiandikisha likiisha wanafanya data exportation kutoka kwenye bvr kwenda kwenye centra data base
 
unaweza kujiandikisha zaidi ya mara 100 kama utatumia bvr tofauti tofauti kwasababu wakati wa zoezi la kujiandikisha bvr hazipo connected. ila hauwezi kujiandikisha zaidi ya mara moja katika bvr moja
 
Sio rahisi kwa mashine hizo mtu kujiandikisha mara mbili iwapo amechukuliwa finger print hata kama data hizo hazijaenda central database.Nilikuwa mwandikishaji na siku moja mtu mmoja alikuja kuandikisha kwangu bahati mbaya nilijaribu mara mbili mashine ikawa inadetect kajiandikisha,nilipomuuliza akaeleza kuwa ukweli,na hapo ilikuwa hata majina niliyoandika yalikuwa hayajapelekwa central database kwa kutumia flash wala online.

Itadetect iwapo mara zote amechukuliwa fingerprint vinginevyo haita-detect

Uko sahihi
 
Ile ni kama komputa yenye internet ukishaingiza data tayari zinakuwa kwenye central database kwa hiyo ukigonga dole gumba popote duniani kwenye mashine ya BVR inaonyesha

Hapana ile sio central na ndio maana huwa wanazituma zile data ktk main computer ambayo iko makao makuu
 
Back
Top Bottom