UKAWA UKAWA
Member
- Sep 24, 2014
- 53
- 15
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA HILI MMEKOSEA SANA YANAHITAJIKA MAREKEBISHO MAPEMA
Wakuu,
naamini sote humu ndani tunakumbuka kuwa TUME ya Taifa ya Uchaguzi itaanza Zoezi la KUANDIKISHA Wapigakura kesho Jumanne Tarehe 16/06/2015 kuanzia Saa 2:00 asubuhi kwa Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Mara na Arusha, baada ya kuliahirisha kwa wiki moja inayomalizika leo.
WILAYA YA SERENGETI
Huku Serengeti Mara,
CCM kupitia kwa Watendaji wabovu waliomo Serikalini, tayari wameanza hujuma katika baadhi ya maeneo kwa lengo la kuminya haki ya Wananchi kuandikishwa.
Mfano;
Kijiji cha Nyansurura
ambako ni Makao Makuu ya Kata ya Nyansurura ndani ya Wilaya ya Serengeti, TUME YA UCHAGUZI kupitia kwa Watendaji wake wabovu, wamekwepa kuweka Kituo cha Kuandikisha Wapigakura, licha ya Eneo hilo kuwa na Taasisi za Umma zaidi ya tatu ambazo ni Shule ya Msingi Nyansurura, Shule ya Sekondari Nyansurura, Zahanati ya Kijiji cha Nyansurura, Kituo cha Polisi Mto Mara na Ofisi ya Kijiji cha Nyansurura.
Matokeo yake wametoa Kituo kimoja pekee katika Kijiji kizima chenye Wapigakura zaidi ya 1,300 na wamekipanga katika Eneo ambalo ni pembezoni mwa Kijiji liitwalo Matanka ambako ni mbali karibu Kilomita tano (5Km) kutoka kwa Wakazi wa Vitongoji vingine.
Licha ya Wananchi kulalamikia sana suala hili kwa Watendaji wa TUME waliofika Kijijini kukagua Vituo ndani ya Kata ya Nyansurura, lakini hadi sasa hakuna dalili zozote za Tume kurejesha Kituo katika Eneo hili kwa kigezo kwamba, Wakazi wanaoishi huku wengi wao hawaiungi mkono CCM, hivyo wakipewa Kituo, watajiandikisha wengi waiangushe vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba 2015.
Kwa msisitizo,
tunaishauri TUME ya Taifa ya Uchaguzi chini Mwenyekiti wake Mzee Damian Lubuva, ione umuhimu wa kuweka Kituo kwenye Eneo hili liitwalo Nyansurura (Centre) kutokana na uhalisia wa Jiografia ya Eneo hili, umbali wa Eneo kilipowekwa Kituo cha kwanza yaani Matanka na wingi wa Idadi ya Wapigakura wanaotarajiwa kuandikishwa katika Kijiji hiki.
Mwenyekiti Serikali ya Kijiji,
Kijiji cha Nyansurura,
S. L. P 81,
Mugumu, Serengeti.
Francis Muhingira Garatwa
0785881009/0767881009
Ahsanteni sana!