Busy,Busy,Busy!

mwana wa mama

Senior Member
May 2, 2013
146
40
Wakuu habari zenu!Naomba niwashirikishe ujumbe huu.


Tutawashughulikia Binadamu ipasavyo


‘’Pamoja na mkakati wetu mkongwe wa uchawi unaowagusa wanadamu wote,hii ni semina elekezi kwa mapepo duniani dhidi ya wakristu na ndoa zao.


Tumeshindwa kuwazuia wakristo wasiende kanisani.


Tumeshindwa kuwazuia wasisome Biblia zao na kufahamu ukweli.Tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na upendo wa kweli kwa mwokozi wao.Mara wapatapo muungano wa kweli na kristo mamlaka yetu yatakuwa yamefika mwisho.Kwa hiyo waacheni waende kanisani,waacheni waendelea na kudumisha mahusiano na mapenzi ya kweli kwa Yesu kristo.Hiki ndicho ninachotaka mfanye,alisema Shetani:Wataabisheni wasipate kamwe kamwe kushikamana na mwokozi wao na wasifungamane naye kwa siku nzima!’’


‘’Tutafanyaje jambo hilo?’’Mapepo yalimwuliza kwa jazba kiongozi wao wa Motoni.


‘’Hakikisheni wanakuwa BUSY(BUSY=Being Under Satan’s York,maana yake waelemewe na mzigo wa shetani) katka mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao.Pia muanzishe mipango mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao’’,alijibu shetani,


‘’Wapeni kutumia, na kutumia,na kutumia;na kukopa,na kukopa,na kukopa.washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku ,kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na waume zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki,na masaa 10 hadi 12 kwa siku ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha.


Wazuieni wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto wao.Familia zao zikipangaranyika mara nyumba zao hazitakwepa msongamano wa kazi na mawazo.Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha kwamba hawasikii ile sauti ndogo tulivu ya Mungu wao.


Washawishini walize radio au kaseti za muziki kwenye simu popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu.Waache TV,VCR,CD na KOMPYUTA,zikiwazimewashwa kama kawaida majumbani mwao,namhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usiokuwa wa kibiblia mfululizo bila kukoma.Hii itasonga akili na fahamu zao na kuvunja ule muungano na kristo.


Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali kwenye meza zao za kahawa na chai duniani kote.Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani ya fahamu zao kwa muda wa masaa 24.Ingilieni kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.


Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi na majarida na kila aina ya matangazo na habari za vitu na huduma yanayowapa matumaini ya uongo.


Wekeni wanawake warembo sana mitaani na kwenye Televisheni na majarida ili kwamba wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo wan je ndio muhimu,na wasiridhike na wake zao;wafanye wake zao wachoke sana,wasiweze kuonyesha upendo kwa waume zao usiku.Wapeni maumivu ya kichwa pia.


Kama hawatawapa waume zao upendo wanaouhitaji sana,wataanza kutazama kwingine.Hiyo itaparanganyisha familia zao haraka sana.


Wapeni waalimu wa uongo ili wawapotoshe,wasifundishe Injili ya kweli kwa watoto wao na waamini wao.


Wapeni zawadi na kadi za Pasaka ili wasizungumize nguvu za ufufuko kwa Kristo juu ya dhambi na mauti.Hata katika karamu zao wachosheni sana kwa anasa na kuwafanya warudi wakiwa wamechoka sana.Hakikisheni wanakuwa BUSY na kusongwa na mambo kiasi kamba hawapati muda wa kutafakari wema wa Mungu.Badala yake wapeni kutalii kwenye maeneo ya ajabu,matukio ya michezo,matamasha,kumbi za sinema na video.


Wafanye wawe ‘’BUSY;BUSY;BUSY!yaani wasongwe na kusongwa na kusongwa na kusongwa na kazi kwelikweli.Na wanapokutanika kwenye ibada zao za kiroho wafanye waingie katika umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa.Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za Yesu.Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe,wakihatarisha afya zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.Itafanya kazi’’.


‘’Itafanya kazi!Huu ni mkakati kweli kweli.’’Mapepo yaliondoka kwenye mkutano yakiwa na hamu kubwa sana kutekeleza majukumu yao waliyopewa na kuanza kuwafanya wakristo wawe na kukimbia na mambo huku na kuwafanya wakristo wawe na kukimbia na mambo huku na huko,wakawa na muda mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao.Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine kuhusu nguvu za Yesu kristo kubadili maisha ya wanadamu.


Hii ndiyo hali halisi iliyoko leo duniani.Walimwengu wako Busy na malimwengu.





 
Back
Top Bottom