Bush kunani tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bush kunani tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Dec 3, 2011.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  No longer at ease,hayumkini si shwari tena!na kimya kingi kina mshindo mkuu.Ziara za wamarekani hawa ndani ya nchi yetu zina tija kwetu?Hofu yangu isije kuwa tunauza mgodi mwingine kwa chandarua zingine ilihali nchi yetu ikiwa ni muathirika mkubwa wa ugonjwa wa malaria.Uchumi wetu leo unashikiliwa na Mmarekani(madini na nishati ya umeme).Tuna experience na ujio wa wakubwa hawa ndani ya nchi yetu.Tumeona kila ujio wao unakuja na mshindo mkuu ndo maana tunajiuliza kunani Tanzania?Tuna kumbuka ujio wa mama Hilari Clinton,alikaa kwa muda wa siku si chini ya tatu na matokeo yake ni kununuliwa mitambo ya Dowans na kusainishwa kwa mkataba wa kuzalisha umeme kwa kampuni ya kimarekani(Symbion).Lazima ifike wakati tujiulize urafiki huu una tija kwa maendeleo ya taifa au ni kwa wateule wachache waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi ?

  Kuna sababu gani ya rais wa nchi kwenda kumpokea mgeni asiye wa Kitaifa,wakati kuna mawaziri husika?Je ni lini wafanyabiashara wetu waliwahi kufanya ziara nchi Marekani na kupokelewa na ujmbe mzito toka serikali kuu?udhaifu unaotumiwa na wageni hawa ipo siku utakuja kuligharimu taifa letu.Na kama ni suala la utalii wapo wahusika wakuu katika wizara husika wangeweza kufanya kazi hiyo na kumuacha rais akishughulikia majukumu mazito ya kitaifa.Ni jambo la kustajaabisha sana kodi za walalahoi zinatumika kuwakarimu wageni wasio wa kiserikali.Tunaomba serikali itueleze ujio huu wa kimya kimya una tija gani katika maendeleo ya taifa hili,au ndo kaleta kibaba kutokana na safari za mh. rais kwenda kuhemea ?

  Kuna tetesi kuwa African Barrick Gold mine wapo katika mchakato wa kuhakikisha mgodi wa Resolute unaingia ndani ya mikono yao,na kama ndo hivyo waweke mambo hadharani kuliko kunyamaza kimya wakati rasilimali zetu zinatoweka kwa mlango wa nyuma.Unafiki huu wa viongozi wetu utaisha lini,kwanini wasiige mfano wa Mugabe!?Naomba kuawakilisha mniongoze kujua ugeni huu wa kimya kimya una tija kwa taifa letu?
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Marekani wamenunua ikulu, si muda mrefu hata bendera ya taifa itakuwa na kichwa cha bush
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,648
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kwamba alialikwa aje kwenye sherehe za Uhuru wiki ijayo lakini akadai ana shughuli nyingine wiki hiyo hivyo asingeweza ndio maana akazuka wiki hii.
   
 4. Blandes

  Blandes JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Watanzania yetu ni macho,mambo kibao yanayo fanywa na wagen tena ya aibu kisa wawekezaji,Bush kaja kucheck miradi yake tu!hamna msaada wowote kwa watanzania
   
 5. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  US leaders have never been tourists and they will never be! When you see such a high powered delegation coming in our country, there is a contract they are coming to finalize or initialize, that the truth of the matter. He went to Zambia because there is a new leader who need to be pocketed! Literally these guys are owning our country right now!
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tafadhali tuambie Rais wetu anashughulikia mambo gani mazito ya taifa hili na kwa maslahi ya nani? Kama mnaendelea kumuhesabia safari zake za nje basi anabadilika na kutumia safari migeuko kwa kuwaita washikaji wake Tz badala ya yeye kukwea pipa kuwafuata ughaibuni.
   
 7. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako familia ya BUSH ni wamiliki wakubwa wa BARRICK ambayo kwa hapa Tanzania inamiliki migodi minne,Buzwagi,Bulyanhulu,Tulawaka & North Mara.Kwa hiyo amekuja kuangalia miradi ya familia inaendaje.
   
 8. M

  MAJI YA BENDERA New Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa tu - bush alikuwa hapa tanzania toka tarehe 27 alikuwa serengeti grumeti amefanya hunting mpaka season za hunting kuisha ambayo ni tarehe 1 december ndio kaja bongo amevaa suit na ninini! Nyinyi mnafikiri ametokea marekani kumbe alikuwa serengeti grumeti.

  Amkeni vijana tanzania yetu hii.
   
 9. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako familia ya BUSH ni wamiliki wakubwa wa BARRICK ambayo kwa hapa Tanzania inamiliki migodi minne,Buzwagi,Bulyanhulu,Tulawaka & North Mara.Kwa hiyo amekuja kuangalia miradi ya familia inaendaje.
   
 10. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Vipi ile Uranium kule Songea? Na pia hebu nijuzeni jamani, inasemekana huyu Bush hakuwahi kufanya ziara ya muda mrefu nje ya Marekani, Tanzania ilivunja rekodi ni kweli? Na kama amepewa mikataba minono basi Tanzania inatisha kwa milungula mpaka Bush kaingia mkenge?
   
 11. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Re: Bush Rais wa Marekani anakabidhiwa lin? Hati ya aridhi ya Kigamboni?
  Mambo yasiyo ya kweli yanayosemwa mitaani ni hatari pale wale wanayoyasikiliza wanapoyaamini. Bush kaja nchini mwetu kama sehemu ya kufuatilia kwa kuona mafanikio ya miradi ya afya iliyowapa watu wengi uhai ambayo aliiasisi akiwa Raisi. Mtu HUYU Bush kwa aliyoyafanya kwetu alistahili Kukaribishwa kwa heshima na sio kejeli. Hivi wenzetu ambao wanakadiriwa kuwa laki mbili na nusu wanaopata dawa za kurefusha maisha bure wangekua wapi leo? Hapa tusizungumzie wanotumiamdawammseto za malaria zinazopatikana pia kwa bei punguzo. Wandugu tatizo letu la kushindwa kuthibiti mali asili zetu ni letu kupitia kwa viongozi wetu wanaotenda mambo Kama alivyofanya Mangungu Yule mtawala wa Morogoro aliyesaini makaratasi ya Karl peters. Wandugu tuwe na kiu ya kujua mambo kuliko kuishia kuzungumzia mambo yasio ya kweli. Mfano nani mwenye uhakika kwamba Bush hata amewahi kuusikia mradi wa Kigamboni Tanzania? Wajameni acheni utopia
   
 12. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Re: Tz; yatakiwa kumkamata George W. Bush Akiwa ziaran nchini. Je, iawrza?
  Wazo lako linaendana na Mtu asiyefuatilia mambo. Bush akiwa Raisi amesaidia upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi na malaria. Hivi hizo biashara zake zaidi ya juhudi zilizo wazi za kusaidia kupambana na maradhi ni zipi? Nasikitishwa na WATU wasioweza kuelewa kwamba ukiona vinaelea ujue vimeundwa...dawa zipo hospitali kwa kila mmoja wetu kuzipata bure dawa ambazo ilikua Hatuwezi kuzinunua kwa ajili ya bei iliyo juu ya uwezo wetu. Wandugu tunahitaji kuzitafakari habari tunazo pata "Vijiweni". Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Bush aliuza share za mamia ya milioni ya Dola kabla kuingia kwenye siasa hadi kuwa Raisi. Hivi mfanyabiashara mahiri Kama HUYU anahitaji kweli Kupitia mlango wa nyuma ili kufanya biashara? Wandugu tuache UTOPIA
   
 13. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Please understand that the Gorvrnment of United States of America through Presidents Aids Relief Programe has made a huge difference in Health care of people with HIV in this country. One should be careful when trying to suggest that the efforts are for some economical gain for USA. Please understand the difference between the Relief and it's absence is like comparing LIFE TO DEATH. A lot of people would have been part of history had not been for the personal efforts of Presidents Bush and Clinton. Politics and economic aside let's us show appreciation to " the gift of life" from these presidents and their government.
   
 14. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  HARI ZAIDI,KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI.rais angekuwa wa upande mwingine kiimani sasa ivi maneno yangekuwa mengine tena makali sana lakini bora ni waupande wao anashrikiana na MAKAFIRI
   
Loading...