Mara mbili katika matukio muhimu nchini, Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa ushauri ambao huenda tumeanza kuusahau.
Moja ni pale alipowashauri wa Tz kuukubali mfumo wa vyama vingi vya kisiasa - alisema, pamoja na kwamba waliokataa ni wengi, lakini hawa wachache wana umuhimu wake la sivyo tutabweteka na kusinzia tukidhani kwa vile tunapendwa tukaona yote tunayofanya ni sahihi hata pale penye uzembe mkubwa.
Pili aliposhauri kuhusu hatari ya ubaguzi wakati wa mvutano kuhusu muungano alisema, tukikubali kubaguana, hatutaishia hapa, tutaendelea kutafuta nani tumbague hadi tutafikia kujibagua wenyewe!
Leo najiuliza: tumefikia mahali tunaona hakuna umuhimu tena wa mawazo ya wachache hadi tunaingiza mambo ya kuwalazimisha kuondoka?
Pili, kwa huu ubaguzi wa wazi tukishawaondoa hawa kitakachofuata nini?
Ni heri kuwa na mbuzi wa kafara ambaye ukimtoa gharama yake ni ndogo, kuliko kufikia kumtoa ng'ombe mzima kafara, ati kwa vile tulikataa kuwa na subira na uvumilivu.
Mark my words ubaguzi unatoka mtaani kwetu sasa unaingia nyumbani mwetu
Na wala si kesho kutwa...ni kesho!