Busara za Masau Bwire

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Tusipoangalia na kuchukua hatua, mpira wetu wa miguu, badala ya malengo hasa yaliyokusudiwa na huyo/hao, mwanzilishi/waanzilishi wa mchezo huu, utageuka kuwa uwanja wa uwasama, chuki na vita, kwa sababu hizo, katika mchezo huu wa mpira wa miguu, tukashuhudia watu wakiuana!

Malumbano, vijembe, na maneno ya kukashifiana yanayoendelea mitandaoni, upande mmoja ukifurahia na upande mwingine ukichukizwa, binafsi sidhani kama ni malengo, afya na sehemu ya mpira kama wazo na makusudio ya mwanzilishi wake.

Nadhani, waanzilishi wa marumbano hayo, hawana uwelewa na malengo hasa ya uwepo wa mchezo huo tangu wazo la uanzishwaji wake, au wanafanya kwa makusudi kwa sababu wanazozijua wao, ambazo wao wanafaidika nazo bila kujali madhara yake kwa jamii, familia ya mpira na hata Taifa kwa ujumla wake.

Mpira wa miguu, unapendwa na una mashabiki wengi, pengine kuliko mchezo wowote Duniani , na watu wanatumia gharama kubwa sana kwa ajili ya mpira, gharama ambazo walio wengi, ni hasara tu, hakuna faida yoyote wanayoipata, kwamba, wametoa pesa, wazalishe, baadaye wapate faida.Hujiulizi kwa nini wanafanya hivyo!

Wachache sana, wanafaidika katika mpira wa miguu, wachezaji, waajiriwa wengine, wafanyabiashara na makampuni yanayoingia mikataba ya kibiashara na taasisi za mpira huu pendwa kwa lengo la kufanya biashara na kupata faida, lakini, mashabiki walio wengi, wanapata nini zaidi ya kutumia pesa zao nyingi kwa ajili ya mpira!

Hicho wanachokipata walio wengi katika mpira wa miguu (mashabiki), ndicho tunapaswa kukiheshimu na kukiendeleza.

Sisi, wakuu wa vitengo vya habari, maafisa habari na wasemaji wa klabu za mpira wa miguu, tujikite katika kukiendeleza hicho ambacho ni faida kwa walio wengi, kunena kwetu, kwa sababu yoyote ile, kusisababishe mafarakano, chuki, uwasama, magomvi na watu kuuana.

Tumeshuhudia, baadhi ya mataifa Afrika, wakiutumia mchezo huu kama sehemu ya kuwaletea amani, na kuwaleta pamoja, kama watu wa Taifa moja, wanaonia mamoja, wanaoishi kwa furaha, amani na upendo kama ndugu ndani ya Taifa lao.

Kwa yanayoendelea hapa kwetu, mijadala na majibizano yasiyo na staha, unadhani ndivyo mpira wa miguu unavyotaka, nini mwisho wake!
 
Busara baada ya kupapaswa na kupakatwa?????!!!! Kumbuka kauli zako unaposhinda.
 
Back
Top Bottom