Busara za kwenye ndoa

Makau Js

Member
Joined
May 25, 2017
Posts
93
Reaction score
233
Mwanangu

Ndoa ni taasisi au kampuni muhimu sana inayounganisha pande mbili zenye lengo la pamoja na nia moja.
Furaha ya ndoa sio harusi bali maridhiano ya pande mbili yenye kuonesha umoja,mshikamano na upendo wa dhati.

wewe mwanamke
Usifurahi kuolewa ili kutoa nuksi bali furahia ndoa ukijua umempata aliyekuwa anakutafuta na uliyekuwa unamngojea.
Ndani ya ndoa kuna maisha ya zaidi ya uchumba hivyo wakati wa ndoa sio wakati wa kuchunguzana bali ni wakati wa kuishi maisha ya uhalisia huku ukijitahidi kubeba madhaifu ya mwenzio na mwenzio abebe ya kwako huku ukitumia uwezo wako na wake mkitazamia kufikia malengo ya;
- ukuaji
Kuhakikisha malengo mliyojiwekea katika kila idara yanakua.
Kukua kiroho,kiutamaduni (ukuzeni utamaduni wenu binafsi wa familia yenu na sio utamaduni wa familia zingine zilizowazunguka.), kielimu,kiuchumi n.k

Tamani sana ndoa yako iwe mfano wa kuigwa kwa mema na sio kwa mabaya,
Ndoa nyingi sana zimekuwa na mifano mibaya na isiyo akisi tamaduni za kiafrika hali hii inapelekea kuwa vizazi vya kishenzi vingi sana ila kwako tambua kuwa kuigwa kwako kunatokana na ubora wa ndoa yako

.......................itaendelea
 
Kumweka Mungu kwa kila jambo ndo siri ya mafanikio, uwazi,trust,kusamehe,busara,.
Na kikubwa upendo... Ndo vichocheo va kudumisha ndoa,Umesema vyema,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…