Bus la Shukrani

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Wakuu nawasalim,

Naomba kuuliza kwa aliye wahi kusafiri kwenda Dodoma hili bus la Shukrani mbona kama limechoka sana hivi kweli lina mudu mwendo na ndani lipoje?
 
Haa Haa Haaaaa..... Wewe Angalia Matairi , Dereva Na Engine. Body Waachie Watoto. By The Way Kama Uwezo Wako Wa Nauli Ni Mdogo Basi Hapo Ndipo Panakufaa, Kama Uwezo Wako Unatosha Basi Mabasi Yapo Mengi Sana. KIMBINYIKO, AL-SAEDY, HAPPY NATION, ABOOD N.K.

Nakutakia Safari Njema!
 
akuuu mi naenda iringa ila hili bus bwana duu
 

Attachments

  • 1438750435535.jpg
    16.5 KB · Views: 969
  • 1438750467167.jpg
    33.9 KB · Views: 880
Hilo basi kwa speed ni hatari, nakumbuka wakati nasoma udom 2008/2011 niliwahi kupanda siku moja tu lakini huo mwendo ni wa hatari saana, nikasema sitapanda tena. Changamoto nyingine ni siti zake hazina cover yaan unakalia vyuma, uvundo ndani yaani inatokana na uchafu maana gari kama dampo, matundu, wadudu wadogo wadogo wanaoruka na kutambaa, n.k
 

ndio maana linaonekana kama rangi limepakwa zaidi ya mara kumi. sasa najiuliza kama juzi jamaa kakamatwa na kigari cha kubebea mizigo kwa kosa eti body chakavu... sasa huyu mwenye hili bus na anabeba abiria je?
 

Ni kweli ht mm nliwah kupanda miaka hyo wkt niko udom,cjui kwa sasa likoje
 
Naskia hilo bas liko vzur sana barabarani.Mi Mara nyingi huwa napanda kimbinyiko.
 
Hakikisha unamwamvuli endapo mvua itanyesha

Mkuu umenikumbusha siku moja nilikuwa natoka moro kuja dar nikasema ngoja niwahi haya mabasi yanayotoka juu nipitilize nalo badala ya kusubiri ya pale pale. Duh nikapanda basi hata jina nimelisahau...tukafika mikese mvua ikaanza nililowa sana mpaka nikajiuliza niko ndani ya gari au nje. Halafu siti ya mwanzo na zile gari nyingine zimeinama mbele basi maji yote yanatiririka hadi kwenye kiti changu. Nilikwazika nilijuta kiherehere cha kupanda basi lile.
 
Lile basi ni chambo tu, wanasubiri muda ufike ndipo wawatoe roho abiria wao ili wanunue mengine. Hawa matajiri wa mabasi huwa wanaanzaga hivi hivi then mwishowe utasikia basi fulani limepinduka na abiria wote wamekufa.
 
champion 'dodoma wadeka' hili gari lilikuwa linaenda dom na kurudi dar siku iyo iyo.
 

huku kwetu kuna mabasi yanaitwa lushanga yametengenezwa kwa mapipa, ila sijui yana engine ya kifaru cha jeshi! yanakimbia kwenye barabara za vumbi ni hakuna mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…