Nimesikiliza habari moja kwenye media ya kimataifa wakiwa wanashangaa jinsi waamiaji haramu wanavyojitoa muhanga kwenda Ulaya huku wakishuhudia wenzao mamia kwa mamia wakizama baharini na kupoteza maisha.
Mama mmoja mzungu alivyokuwa akihojjiwa alionyesha kuwa na moyo wa huruma sana na anasema (sio official quote) kuwa "nawasikitikia hawa watu weusi wasio na hatia, najitahidi kutoa kila ninachoweza lakini siwezi kuwasaidia wote. Nawashangaa wanasiasa wa hapa Ulaya na huko wakimbizi hawa wanakotokea wanafanya nini kuwafanya hawa binadamu pia kujiona kama sehemu ya dunia"
Huyo mama kanikumbusha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pale alipotoa angalizo kuwa Waafrika tusipoangalia mabeberu watatufanya kama wanyama walioko Serengeti! Nasikitika kuona kuwa hata Nkurunzinza anachangia kushusha hadhi na heshima ya Mwafrika!