Buriani waungwana

Buriani waungwana

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,499
Buriani waungwana, limenipata dubwana,
Mapema tunaagana, Ningali bado kijana,
Maumivu yanibana, kuandika nangangana,
Buriani waungwana, limenipata dubwana,

Sina wa kumpa lawama, hata Zerea kimwana,
Akijua sana vyema, kalizoa Dubwana,
Kama na kosa kusema, nisamehe tu Rabana
Buriani waungwana , limenipata dubwana,

Simanzi imenitanda, Giza ti likitanda,
Siwezi tena kutenda, siku nzima tu kulala
Nimechoka nimekonda, nipumzike ndio sala
Buriani waungwana , limenipata Dubwana

Malengo yamezimika, kama nta yayeyuka,
Sijui kama ntafika, hata kesho kunyanyuka,
Tumaini lakatika , kiama kinanifika,
Buriani waungwana, limenipata dubwana

Kama vile mnaniona, mwovu kupita kipimo
Ajuae ni Rabana, kwake nafanya ungamo
Nazidi kuchoka sana, niondoke tu nilimo
Buriani waungwana, limenipata dubwana

Kwaherini Marafiki, wangu wa nema na dhiki,
Hata wale wanafiki, chekeni sasa mna haki
Dubwana hakabiliki, kifo hakiepukiki,
Buriani waungwana, limenipata dubwana

Wazazi na ndugu zangu, musiwe na mfadhaiko
Ni mapenzi yake Mungu, hakunalo badiliko,
Pokeeni tu japo chungu, kwake nipate pumziko
Buriani waungwana, limenipata Dubwana,

Kwaherini Duniani, Tuonane bandarini,
Kwaherini jamiini, na hata kule Twitani,
Na kote mitandaoni, niwaage kwa amani
Buriani waungwana, Tutaonana baadae
 
Back
Top Bottom