Buriani Salima

Buriani Salima

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,829
Reaction score
3,733
MUANDISHI: Dawa yenu
STORY: BURIANI SALIMA

Mapenzi ni kama ushairi, ushairi wa huba wenye beti murua zilizosukwa kiustadi na kupangiliwa kwa urari wa vina na mizani. Mapenzi ni zaidi ya bustani, bustani nzuri ya maua yaliyochanua vyema na kuipamba nafsi kwa rangi zenye kuvutia. Mapenzi ni mfano wa tunda tamu, ladha yake aijuaye mlaji. Asali haiwezi kufikia tamu ya mapenzi, sukari haiwezi kufikia tamu ya mapenzi. Hii ni simulizi yangu ya mapenzi.

Moyo wangu uliridhia kisha nafsi ikanikubalia kuwa yeye ndiye wangu maridhia. Utamu alionipa hakuna wa kuufikia. Kila tulipoonana kwa huba alinikumbatia, busu akanipatia, kwa bashasha nikalipokea. Mbele ya macho yangu alikuwa zaidi ya malkia, kuwa naye nilijivunia. Yeye alikuwa wangu msiri, yeye alinifukiza kwa uturi, alinikanda kwa asali, penzi lake mahiri alinipa lote pasina ubahiri.

Salima, alinifanya nijihisi mgeni wa mapenzi. Alinifanya nitamani kurudi darasani nikajifunze namna iliyo bora ya kumuenzi. Nilitamani kurudi darasani nikajifunze namna ya kumpenda zaidi maana kila nilipompenda nilihisi kama haitoshi. Nilimpenda yeye, nilimpenda sana na nilipenda kila kitu kuhusu yeye. Nilimpenda vile alivyo na nilimpenda vile asivyo. Niliyapenda madhaifu yake maana bila hayo huenda asingekuwa yeye, Nilimpenda my darling. Nilimpenda yeye.

Ni muda mrefu umepita, ni muda mrefu sana ila bado naikumbuka vizuri ile siku. Ni kama ilikuwa jana tu maana nakumbuka kila kitu! Nakumbuka kila tukio. Abadani siwezi kuisahau maana ni siku iliyoweka alama ya pekee katika historia ya maisha yangu. Tabasamu huipamba sura yangu kila niikumbukapo siku ile, siku pekee ya kukumbukwa! Ni siku isiyosahaulika katika maisha yangu ya chuo.

Moyo wangu ulisimama kwa dakika kadhaa. Damu ikaacha kuzunguka ndani ya mwili wangu, vipele vya matamanio vikanitoka. Mboni za macho yangu zilikuwa zikitalii kwa ustadi juu ya maungo ya malkia huyu. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona Salima, sikuwahi kumuona kabla ya hapa. Alikuwa kwenye mgahawa wa chuo, alikuwa amekaa na wenzake wakipata staftahi huku utani na vicheko vikiwa vimetamalaki baina yao.

Salima alikuwa amevaa fulana nyepesi sana yenye rangi ya pink na sketi fupi ya rangi ya nyeusi yenye mpasuo mwanana uliopelekea mpasuko wa ashki zangu za huba kwa kuwa uliacha nusu ya mapaja yake yaliyonona mithili ya chungwa bivu yakiwa hadharani. Hakika Salima aliutikisa moyo wangu.

Tabasamu lake la ashuo, lafudhi ya kileo, nyonga yake ya mwambao, nywele za kifilipino, cheko la kireno, pozi kama Muitaliano basi mie hoi taabani sina neno. Macho yake makubwa wastani yalilegea kama anataka kulala, guu lake chupa bia, shingo yake ya upanga, kiuno cha kuvalia shanga, kifuani saa sita, vidole vyake laini kama Margarita. Ilikuwa burudani kumtazama. Sauti yake kinanda utadhani anakubembeleza. Anapozungumza na kuyapangilia maneno kwa ufundi utadhani Jacquline Wolper au Irene Uwoya yupo location. Hakika hakuna maneno yenye kutosha kueleza hata nusu ya sifa za Salima.

Nakumbuka ilivyokuwa. Nitakusimulieni kila kitu. Taratibu kwa adabu na staha zote niliwasogelea na kila mmoja nikampa mkono wa salamu ila nilistaajabu, Salima alikataa kunipa mkono. Kwa dharau akanitazama, kwa nyodo akanipandisha na kunishusha kisha akaendelea kula chakula chake. Si tu alinidharau bali alinivua nguo mbele ya kadamnasi. Aliniaibisha.

Nilikosa raha, nilikosa amani, sikuwahi kuumia kama nilivyoumia siku ile. Wenzake wote waliona tukio hili ila hawakutia neno. Niliona dunia imenitenga, walimwengu waliniacha niadhirike, hawakunitetea. Niliondoka taratibu huku nikimuomba Mungu anisaidie, anipe nguvu ya kuisahau dhahma hii.

Dakika zilipita, masaa nayo yakasonga, ikawa siku, wiki, miezi na hatimaye tukaumaliza mwaka huku tukio lile likiwa kama kivuli changu kuna muda kinapotea na kuna muda kinarudi. Haikuwa rahisi kwangu kuisahau aibu ile. Sijawahi kuaibika vile.

Chuoni pilika nyingi, harakati nyingi zisizoisha na hatimaye nikajikuta katika ulingo wa siasa. Ulikuwa ni wakati wa aina yake, mambo yalikuwa moto, figisu na fitna za kila aina ila kwa mapenzi ya Mungu, jitihada za marafiki na uwezo binafsi hatimaye nikaingia katika serikali ya wanafuzi na jumuiya nzima ikanitambua kama waziri wa habari na mawasiliano na huo ukawa mwanzo wa majukumu mapya chuoni.

Nakumbuka ilikuwa siku ya jumapili, nikiwa katika ofisi yangu ya wizara ya habari ghafla simu yangu ya kiganjani ikaita. Ilikuwa namba ngeni. Nilipopokea nikakutana sauti tamu zaidi ya asali. Alikuwa binti akihitaji muongozo wa kuandika barua ya kuomba kutofanya mitihani maana anataka kusafiri amepata matatizo, alisema amefiwa na baba yake. Roho ya huruma ikanijaa ndani yangu, kwa upole sana nikamwambia aje ofisini ili nimpe mfano wa barua hiyo.

Baada ya dakika kumi mlango wa ofisi ulifunguliwa kisha akaingia binti ambaye alinifanya nitetemeke, huku vipele vya baridi vikichomoza katika ngozi yangu na chuki ikionekana kuishinda nafsi yangu. Akaingia, akakaa kwenye kiti mbele ya meza yangu, macho yake mekundu, hana amani, amempoteza baba yake. Salima alikuwa mbele ya macho yangu, tupo wawili tu ofisini.

Hali yake ilikuwa mbaya, nikasema na roho yangu. Nikazungumza na Mungu wangu, busara ikarudi ndani yangu, nikampa maelekezo yanayostahili huku nikimpa maneno yenye kumpa nguvu maana msiba hauzoeleki na hakika kila mwenye kufiwa anastahili faraja. Baada ya maelekezo akaandika barua kisha siku ya pili akasafiri. Nakumbuka jioni ya siku hiyo nilipigiwa simu na Salima akaniambia kuwa amefika kwao salama ila amekuta tayari wamezika.

Taratibu, polepole ikageuka kuwa mazoea, haiwezi kupita masaa kadhaa bila Salima kunipigia simu. Tukajenga urafiki, akawa rafiki mzuri kwangu. Basi nikamsimulia alichonifanyia siku ile, akacheka sana ila akaniomba msamaha huku akiahidi kutofanya tena kwa mtu mwingine, akasema alikosea sana ila sasa amejifunza.

Aliporudi chuo akanitafuta tukazungumza sana! Akasema ninampa furaha sana. Tukawa karibu hakuna mfano kila sehemu tupo pamoja. Ni hapo ndipo nilipoanza kuhisi tuvitu vitu kuhusu yeye, nikaanza kumtazama kwa namna tofauti, aliniingia moyoni Salima, aliniingia bila kupiga hodi, nilimpenda kwa dhati ya moyo wangu. Nilimuhitaji kimapenz ila kinywa changu ni kama kilifungwa.

Nikiwa kama kiongozi wa serikali ya wanafunzi, chuo chote kilikuwa kikinifahamu hivyo habari zikaenea kwa kasi ya kimbunga kuwa hatimaye waziri amepata jiko. Story ilikuwa kubwa na hatukuwahi kukataa wala kukubali na ajabu zaidi hatukuwahi kujadili kuhusu hilo.

Tuliishi kama wapenz ila hatukuwa wapenzi na hakuwahi kunionyesha dalili zozote kuwa ana mahusiano. Kuna siku nikapata habari kuwa ameonekana mjini na mshkaji flani na huyo jamaa namjua ni kiwembe hatari. Nilikasirika zaidi ya simba aliyejeruhiwa. Nikajiapiza kuwa akirudi ataujua moto wangu ila sikujua huo moto nitauwasha kama nani? Nitauwasha kama mpenzi au kama rafiki? Nikiuwasha kama mpenzi je yeye ni mpenzi wangu? Nikiuwasha kama rafiki je nina mamlaka hayo? Vyovyote itakavyokuwa ila moto lazima niuwashe, ataendaje mjini bila kuniaga?

Jioni ilipofika nikaenda chumbani kwake, alikuwa anaishi peke yake karibu na chuo. Nikamkuta anajiandaa kulala! Nilimfokea sana, nikamwambia hayupo makini ana tabia mbaya sana. Hajali afya yake yaani amenishangaza sana, nimeambiwa anatoka na yule jamaa! Nikamuuliza kwanini hakuniambia anatoka na yule jamaa ili nijue?

Alinishangaa sana, hakunielewa ila akanieleza kuwa hana mahusiano na yule jamaa. Ni kweli alikuwa nae mjini ila walionana huko huko mjini na kila mtu alikuwa na mishe zake na hizo story nilizopewa ni za uongo na kama siamini basi tumpigie simu yule jamaa tumuulize. NIKAKATAA KIBABE! Ila angalau munkari ulikuwa umetulia.

Tulikaa kitandani tukapiga story nyingine nyingi ila swali lake kubwa lilikuwa ni kwanini nimekasirika kuambiwa kuwa yeye ana jamaa mwingine? Akaniuliza kwanini nina wivu, kwanini imekuwa vile? Nilijaribu kujitetea kuwa namjari sana, sipendi apotee ila hata mimi nilijua sina hoja za msingi. Nakumbuka alinitazama usoni kasha akaniambia,

“Suleyman, kama ambavyo umeumia kusikia nina mwanaume, ndivyo nitakavyoumia nikisikia una mwanamke zaidi yangu” sikujua kama nimemsikia sawasawa na kumuelewa ila nilitabasamu kisha nikachukua simu yangu huku nikijiandaa kuaga.
“Suley…. bhana lala hapahapa” aliongea kwa deko na manung’uniko huku ananishika kifuani kwa huba na bashasha tele.
“Umesemaje?” Niliuliza huku nikiwa nina mashaka juu ya kile nilichokisikia, hivho ndicho alichosema au masikio yangu yananidanganya?
“Au hutaki kulala na mimi jamani” aliongea kwa hisia kisha akavuta pumzi na kuendelea, “Bhana leo nifanye chochote unachojisikia…. Nina hamu na wewe… come on baby”

Dakika mbili zilizofuata tulikuwa juu ya shuka jeupe la kitanda chake. Kwa mahaba tele alinibusu shingoni, akanilamba sikioni, akaninyonya mdomoni, nikamtomasa maungoni, nikampapasa kiunoni, nikamtuliza kifuani ikawa burudani na akasema hajawahi kufanywa mfanyo kama ule, mfanyo usio kifani, mfanyo ulioenda shule.

Tukawa kama vipepeo kila sehemu tupo wote, nakumbuka tulishona hadi sare kusindikiza utamu wa penzi jipya. Tupendana sana ila kuna jambo halikuwa sawa. Kuna jambo lilikuwa likinishangaza kuhusu Salima. Alikuwa anaumwa mara kwa mara na hakuwahi kuniambia anasumbuliwa na nini. Nakumbuka siku moja alizidiwa sana ikabidi arudishwe kwao na hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho kumuona Salima wangu.

Alipoondoka mawasiliano yetu yalikuwa ya shida sana. Meseji zangu hakuwa anajibu kwa wakati na hata simu zangu alipokea pale alipojisikia. Niliumia ila sikukata tama hadi pale aliponitumia ujumbe mfupi wa maandishi.

”Suleyman naomba unisamehe sana. Nimeishi nawe muda mrefu na nikaruhusu unipende huku nikijua mwisho ya haya yote ni maumivu makubwa kwako. Suley nakupenda ila mimi si wako. Maisha yangu ni mafupi sana nina kansa ya damu. Sasa ninakufa mpenzi wangu. Siku ile niliikataa salamu yako ili unichukie, nilitaka usinipende ili nisije kutesa hisia zako ila ilishindikana. Suley pole sana ila naamini utanisahau. Bye.”

Sikutaka kuelewa ujumbe wake una maana gani, nikachukua simu kisha nikampigia ila simu haikupokelewa. Nilipiga tena na tena ila simu haikupokelewa. Nilijihisi mnyonge sana ila Mungu si Athumani jioni ya siku hiyo Salima alinipigia simu. Nilipata amani kidogo ila nilipopokea kumbe hakuwa Salima wangu bali alikuwa dada yake. Huku akiwa analia kwa kwikwi akaniambia,

“Suley, Salima alikuwa anakupenda sana, tutamzika kesho kutwa. Tafadhali fanya hima uhudhurie mazishi yake.”

MWISHO

“Mahusiano imara ni matokeo ya mawasiliano imara"

Dawa yenu, 2020
IMG_20200301_072929_566.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom