Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,454
- 32,980
BURIANI MWANETU AWADH MOHAMED AWADH
Awadh Mohamed Awadh (Chico) alikuwa kafanana sana na baba yake.
Mimi sikupata kumwita kwa jina lake la Awadh kwangu alikuwa Chico sijui kwa nini.
Labda kwa kule kurandana sana na baba yake.
Wazazi hatupendi kuzika wana.
Hatupendi kwa kuwa ni jambo zito na gumu sana lililojaa simanzi kubwa.
Lakini nani wa kushindana na Kadar ya Allah?
Nilikuwa kila tukionana katika shughuli basi nitamwambia ni kwa kiasi gani mimi na baba yake tulivyokuwa marafiki utotoni kuanzia Everton hadi Saigon.
Kitu kimoja kimenikaa moyoni.
Mwanangu alikuwa anakwenda kusoma nje ya nchi na pakatakikana barua kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kuwa hana rekodi ya jinai.
Muda wa chuo kufunguliwa ulikuwa unakaribia.
Mambo haya yana ugumu wake.
Huwa panda shuka lete hiki lete kile.
Muhusika kasafiri inabidi tumsubiri nk.
Siku hiyo namueleza Baba Juma, Boi Risasi wa Saigon kuhusu kizingiti hiki.
Boi bila kupepesa akanambia, ''Nenda Wizarani kamuone Awadh Chico.''
Mimi sikupanda juu kumuona Awadh.
Nilibakia kwenye gari chini nikamwambia mwanangu, ''Huyu ni kijana mwenzio nenda mwenyewe ukamweleze shida yako kujuana ndiko huku mimi nakusubiri hapa chini.''
Haukupita muda namuona mwanangu karejea na tabasamu kubwa mkononi kashika barua.
''Baba Awadh anakusalimu sana.''
Wenzake wananiambia Awadh hakuwa mbali na dini yake na alikuwa na mapenzi makubwa na Walimu wa Qur'an.
Inatosha.
Allah mpokee mja wako na mfanyie wepesi safari yake.
Amin.
Picha hizo hapo chini nilipiga kwenye khitma ya baba yake marehemu Awadh, Kamanda Chico mwaka wa 2017: