Mkuu siku hizi thamani ya exports zetu ni ndogo kuliko imports. Tumefikia mahali tunaagiza kutoka nje meza, viti, etc. Hatutaki kutumia mbao za humu nchini. Kilimo cha mazao kama pamba, kahawa, korosho, mkonge etc kilisha dorora miaka mingi iliyopita kwa sababu ya jembe la mkono. Achana na porojo za "Kilimo Kwanza" maana hii ni gear ya kura za 2010. Mikataba ya madini imefanya tusiambulie chochote kwenye dhahabu. Hata hiyo Uranium mambo yatakuwa vivyo hivyo. Bado tunaagiza magari, mitambo na safari za majuu za vibosile wa nchi zinatafuna akiba kidogo ya fedha za kigeni tuliyonayo. Sasa ukitaka kununua dollar kwa hela zako za madafu ni lazima utauziwa kwa rate ya juu mwanangu. Thamani ya Shilingi yetu kwishnei bana.
Nikisoma maelezo yako kitu kinachobakia kama sababu na guarantee ya thamani ya pesa ni SIASA za hii nchi yetu na matendo ya Wanasiasa kwa ujumla. Au, kuna kingine tena...?...Ila kwa maneno ya jumla zaidi ni kwamba uchumi wa nchi ndio una-act kama guarantee ya value ya currency ya nchi husika.
Chochote kingine utakachojaribu kufanya (kudhibiti nani anaweza kununuafedha za kigeni, etc) kunaweza kukaonekana kama kusaidia ku-stabilizie currency ya nchi. Lakini in the long run, haitasaidia kama uchumi wa nchi si mzuri.
...
Kwa hayo pengine unaweza kuona kwamba, hata tuki-export vitu vichache, bado kuna uwezekano wa kuwa na currency ambayo inathamani. La sivyo ingebidi tuhitimishe kwamba nchi ambayo hai-export chochote basi fedha yake itakuwa haina thamani kabisa, kitu ambacho si kweli pengine
Maelezo murua kabisa hayo mkulu Manitoba. Ahsante.
Nikisoma maelezo yako kitu kinachobakia kama sababu na guarantee ya thamani ya pesa ni SIASA za hii nchi yetu na matendo ya Wanasiasa kwa ujumla. Au, kuna kingine tena...?
Kabisa mkuu.
Sera ya fedha ndiyo inatumiwa ku-control thamani ya pesa pamoja na ukuaji wa uchumi (http://en.wikipedia.org/wiki/Monetary_policy ). Na siasa mkono wake unafikaga huko ... so u see the link. Sera ya fedha yaweza kutmika vibaya kwa manufaa ya kisiasa, au ya watu wachache wenye influence na kusababisha mengi tu ikiwa ni pamoja na kushuka kwa thamani ya fedha au hata kuporomoka kwa uchumi.
Ahsante Manitoba kwa maelezo yako mazuri. Kwa Tanzania sera ya fedha na utekelezaji wake haufanywi inavyotakiwa. Mathalani moja ya mashtaka ya wakubwa wa BoTwaliofikishwa mahakamani juzi ni kuchapisha hela in eccess. Kwahiyo ile calculated reserve haiwezi kulingana na hela iliyoko kwenye mzunguko kwa sababu kuna mianya mingi ya kuingiza fedha chafu kwenye huo mzunguko.
Suala la bureau de change linakuja kutokana kwamba anayepata hizi hela nyingi nje ya utaratibu atataka kuzihamishia nje ya nchi zikiwa in form of dolar or euro etc. Historia inaonyesha waafrica wanapenda kuficha mahela yao nje.
Nadhani kuna point ya kuhighlight pia. Serikali ndio msimamizi na mmiliki wa benki kuu. Sasa benki kuu wakisema akiba yetu ya fedha ya kigeni natosha miezi nane, wanamaanisha mkopo??? Nadhani jibu ni hapana. Naomba ni tofautiane na wewe kwahili si kwamba serikali hawana pesa, wana pesa na wanamamlaka hata ya kuprint fedha ya ziada. Lakini sasa wakiprint hiyo fedha, effect yake ndio inflation uliyoitaja na in the end consumer wanaloose appetite ya local currency.Off topic kidogo, lakini kuna-kitu kimoja interesting ambacho wengi hatukijui: fedha zako inwezekana si zako. Hata serikali yako haina pesa. Pesa zote unazoziona ni mikopo.
Hebu jiulize, serikali ikitaka pesa inafanyaje? Inakopa kutoka kwa benki kuu au kutoka kwa watu binafsi kwa kupitia benki kuu, na riba kubwa tu. Cha kushangaza hapa ni kwamba serikali ambayo pengine ndiyo ingebidi iwe mmiliki wa hizo pesa inabidi ikope na tena ilipie mkopo huu riba.
Serikali inapata wapi pesa sa kulipa deni hilo? Ni kwa kutukata sisi kodi. Ndio maana sehemu ya kodi tunayolipa lazima iende kwenye kulipa deni hilo, na inayobaki ndio tunaigawa-gawa kwenye bajeti.
Kwa hiyo serikali yetu huwaga haina pesa. Sasa kama haina pesa je, supply ya fedha huwa inakuwa controled vipi?
Kumbuka supply ya fedha ikiwa kubwa kuliko ambavyo uchumi unaruhusu tuna inflation kwa sababu thamani yake inshuka. Supply ikiwa ndogo, tunakuwa na deflation ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi.
Unaweza ukalia ukijua ukweli.
Ili ku-control inflation inabidi kuondoa fedha kwenye mzunguko. Kufanikisha hili inabidi kupunguza matumizi yake. Na tunajua jinsi hii inavyokuwa tofauti na malengo ya kisiasa.
Ili ku-control deflation inabidi kuongeza pesa kwenye mzunguko. Lakini kwa kuwa serikali haina pesa, inabidi kwenda kukopa tena. Na hiyo inamaanisha riba inaongezeka. Itatoa wapi hii riba? Tunakamuliwa kodi!
Sasa kuna watu wachache ambao wao wanakula kuku kwa mrija. Kazi yako ni kuikopesha serikali na kusubiri riba. Hawa watu hawawezi kulala njaa kwa sababu serikali tayari iko kwenye deni na haina pesa, na inahitaji kukopa.
Sasa jiulize hawa watu wanatoa wapi pesa za kuikopesha serikali ambazo haziishi?
Pengine tujiulize hawa watu ni wakina nani? Kwanza ni Benki Kuu lakini kwa hapa TZ Benki kuu tunaweza kusema ni ya serikali (pengine kwa kuangalia juu juu), kwa hiyo pengine tuko safe kuliko wamarekani kwa mfano. Pili ni mabenki.
Hivi unajua mabenki yanatengeneza fedha? Nnaposema kutengeneza fedha simmanishi kuzalisha kama tunavyomaanisha tukiwa mtaani. Namaanisha ni kama vile kuchapisha pesa, na kuziingiza kwenye mzunguko
Chukulia wewe n benki, na ukapokea deposit ya buku moja, 1,000TZS kutoka kwa mteja M1. Mteja M2 anakuja anataka mkopo wa 900TZS. Unampa 900TZS. Kwa hiyo M1 anasema na 1,000TZS na M2 akiulizwa anasema na 900TZS. Jumla una 1,900TZS. Kwa bahati M2 ana-deposit hiyo 900 yake kwenye account iliyo kwenye benki yako. Anakuja M3 naye anataka 800TZS. Kutoka kwa 900 ya M2 unatoa 800 unampa M3. Mpaka sasa tuna 2,700TZS. Kwa hiyo benki yako kwa kupokea 1,000TZ ya deposit imeweza kutengeneza pesa kiasi cha 1,700TZS na kukiingiza kwenye mzunguko. Na hapo sio mwisho.
Na utamu hapo ni pale mteja anayefuata (M4) anapokuwa serikali, utakosa pesa ya kuikopesha?
Na unaweza kuta hata ile 1,000TZS ni pesa ambayo engineer flani amelipwa na mkandarasi kwa pesa ambayo imetoka kwa serikali, ambayo serikali imekopa kutoka kwa benki yako.
Sasa hapo utaona jinsi gani banks na sio bureau de change zinaweza kusaidia inflation kwa sababu wana uwezo mkubwa zaidi wa kutengeneza fedha (yaani ni kama ku-print notes).
Tunajua kwamba ongezeko la money supply ndio linalosababisha inflation. Yaani kunakuwa na pesa nyingi zaidi ya zinazohitajika kwa ajili ya kuimarisha bei za vitu. Na kwa kuwa mabenki yana uwezo kwa kutengeneza pesa, na uwezo huu upo nje ya uwezo wa serikali, utaona kwa nini inaweza kuwa ngumu sana saa nyingine kwa serikali ku-control inflation.
Kwa hiyo ukiona watu wanakuwa-encouraged sana kukopa, anza kuangalia kwa mtazamo tofauti kidogo. Waofaidika kwa kiasi kikubwa ni mabeki wakati sisi wengine wote tunaingizwa kwenye madeni, hasa pale pesa hizi zinpokuwa zinazunguka bila kuzalisha.
Nadhani kuna point ya kuhighlight pia. Serikali ndio msimamizi na mmiliki wa benki kuu. Sasa benki kuu wakisema akiba yetu ya fedha ya kigeni natosha miezi nane, wanamaanisha mkopo??? Nadhani jibu ni hapana. Naomba ni tofautiane na wewe kwahili si kwamba serikali hawana pesa, wana pesa na wanamamlaka hata ya kuprint fedha ya ziada. Lakini sasa wakiprint hiyo fedha, effect yake ndio inflation uliyoitaja na in the end consumer wanaloose appetite ya local currency.
Labda kucement hii point, nadhani ipo haja ya kufaham kuwa katika finacial markets (masoko ya fedha), utaona securities (dhamana) za serikali zinakuwa a return( interest), riba kidogo. Sababu kubwa ni underlying assumption that the government cannot default. Maana yake ni kwamba serikali kama ilivyo inauwezo wa kuprint notes, pesa za ziada pale itakapohitajika kulipa na ndio maana risks iliyopo kwenye dhamana zake huwa ni ndugu kuliko dhamana binafsi na za makampuni na hata hiyo riba inabidi iwe kidogo. Kwahiyo serikali inuwezo wa kutengeneza fedha ya ziada, rejea ishu ya zimbambwe na kwa maana hiyo serikali inaweza kuwa na pesa but while accounting for fiscal and monetary policy.
Hoja ya bureau, mfano wako ni mzuri saaana. Lakini kwa wale wanaosema bureau zinatumika kuhamisha pesa, hapana hii si kweli kuna procedures zimeongezeka tokea March mwaka huu hata kutransfer pesa nje inayozidi 10mil BOT wanahitajika kuidhinisha. Kwahiyo ishu is rahisi hivyo. Labda ukizungumzia issue ya speculation kwa hawa wanaofanya bashara ya pesa inaweza kuwa sahihi na hii inafanywa popote duniani ila Tanzania u can always bet the market b'se the market itself has never been efficiency.
Suala la KILIMO KWANZA ni technique nzuri saana kuinua uchumi wa nchi yetu kama tu siasa itawekwa kando. Tukweza kuzalisha na hata tusiwaze kuuza Ulaya na Marekani, bado Afrika kuna msoko ya kutosha kwenye vyakula. Jirani zetu hapo Kenya, they have always been starving. Ukweli kwenye kilimo bado kuna opportunities.
Natambua limemlenga Manitoba lakini naomba kuchangia. Dollarization ni matokeo tu, ila behind dollarisation ndio kuporomoka kwa shilingi. Shilingi ingekuwa stable dollarisation isingekuwepo. Refer Zimbabwe. Lakini shilingi imekuwa weak na watu wanafanya biashara zao kwa kuimport raw materials na other products. Sasa unaimport leo just after days vitu kabla bidhaa haijafika exchange rates zinabadilika, unategemea nini. Hapo ndio maana watu wakaopt kwa dollarisation. Lakini option hii ndio ikafanya hali ya shilingi iwe mbaya zaidi maana hakuna anayetaka kuitumia, kwa maneno mengine dollarisation has created weak demand for Tsh. Hapo kazi ikaongezeka people are shunning away from Tshs. Inamaana Tsh is becoming cheaper na ndio matokeo yanayoonekana.Manitoba,
Swali - je ni nini kisababisha chenzake kati ya doralization* na kushuka kwa thamani ya TZS? Je ni doralization ndio inachangia thamani ya hela yetu kudorola au ni thamani ndogo ya hela yetu ndio inasababisha doralization?
*doralization - tabia ya baadhi ya watu nyumbani kupanda bei kwa kutumia dollar.
Manitoba,
Swali - je ni nini kisababisha chenzake kati ya doralization* na kushuka kwa thamani ya TZS? Je ni doralization ndio inachangia thamani ya hela yetu kudorola au ni thamani ndogo ya hela yetu ndio inasababisha doralization?
*doralization - tabia ya baadhi ya watu nyumbani kupanda bei kwa kutumia dollar.
Hiyo kaka ni nadharia tu. Nadhani we need to ge back kuangalia roles za central banks. Uhusiano wangu na CRDB au NMB haulingani kamwe na BOT. Nani anasimamia BOT? Utagundua ni serikali. Policies zote za fedha zinaandaliwa na BOT, unadhani kwanini? BOT ni entity ya Serikali, ukijitahidi kuwatofautisha ni kinadharia tu. Ndio maana hata dhamana za serikali na kucontrol money circulation hiyo kazi inafanywa na BOT kwa niaba ya serikali is nt about Banker. Inamaana taarifa ya benki kuu sio ya serikali. Mf Akiba ya fedha ya kigeni tunachokiasi kadhaa......... ni kina nani kama si serikali?Kwa fedha za kigeni, mfano uliotoa unaonyesha kwamba BOT ni banker tu wa serikali. Je wewe CRDB akiwa ni banker wako, haiwezekani account yako ya dolar ikawa positive wakati account yako ya TZS ikawa negative? Je, hata kama una account moja mbili zilizo positive, haiwezekani jumla ya pesa ulizo nazo kwa benki hiyo zikawa negative (kama kwa mfano kuna account ome overdraw kupita kiasi?
BOT waki-print fedha kuna mawili.
Kwanza kuna ku-replace fedha zilizochakaa. Fedha zilizochakaa zinarudishwa BOT na BOT wanatoa fedha mpya.
Pili, serikali ikipewa pesa na BOT nje ya pesa zilizo kwenye account za serikali ndani ya BOT, haipewi bure baba. Inakopeshwa kwa riba. Uhusiano wa serikali na BOT hauna tofauti na wewe na CRDB au NMB kama banker wake. Ila kwa sababu siasa zetu zinaruhusu muingilione, then tunaweza tukadhani kila kilichopo BOT ni cha serikali. Na tushaona madhara ya muingiliano huu.
Natambua limemlenga Manitoba lakini naomba kuchangia. Dollarization ni matokeo tu, ila behind dollarisation ndio kuporomoka kwa shilingi. Shilingi ingekuwa stable dollarisation isingekuwepo. Refer Zimbabwe. Lakini shilingi imekuwa weak na watu wanafanya biashara zao kwa kuimport raw materials na other products. Sasa unaimport leo just after days vitu kabla bidhaa haijafika exchange rates zinabadilika, unategemea nini. Hapo ndio maana watu wakaopt kwa dollarisation. Lakini option hii ndio ikafanya hali ya shilingi iwe mbaya zaidi maana hakuna anayetaka kuitumia, kwa maneno mengine dollarisation has created weak demand for Tsh. Hapo kazi ikaongezeka people are shunning away from Tshs. Inamaana Tsh is becoming cheaper na ndio matokeo yanayoonekana.
Hiyo kaka ni nadharia tu. Nadhani we need to ge back kuangalia roles za central banks. Uhusiano wangu na CRDB au NMB haulingani kamwe na BOT. Nani anasimamia BOT? Utagundua ni serikali. Policies zote za fedha zinaandaliwa na BOT, unadhani kwanini? BOT ni entity ya Serikali, ukijitahidi kuwatofautisha ni kinadharia tu. Ndio maana hata dhamana za serikali na kucontrol money circulation hiyo kazi inafanywa na BOT kwa niaba ya serikali is nt about Banker. Inamaana taarifa ya benki kuu sio ya serikali. Mf Akiba ya fedha ya kigeni tunachokiasi kadhaa......... ni kina nani kama si serikali?
Hv unadhani tumefikaje kwenye notes za TSh 10,000. Hii ni madhara ya inflation ambayo yanauhusiano na extra notes printing. Ingekuwa wanareplace tu?????
Very true inawezekana tatizo likapungua. Lakini impact yake sasa inawezekana kuwa kubwa zaidi ya kuzuia matumizi ya dollar. Maana hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kuuza kwa hasara. Hata kama ukiamua kutumia Tshs, curency yenyewe sio stable inamaana utabadilisha bei mara ngapi. Je customers implication inakuwa wapi hapo? Cha kufanya ni kutokimbizana na wafanyabiashara. Wao wahakikishe wanasound Macro economic policy. Ikibidi hata intervention ingawa sio proper approach. Angalia Japan na China, wao wanaintervene saana fadha zao ndio maana Marekani wanalalamika kila asubuhi.Kama nimekuelewa vizuri - kwa hiyo mwanzo ilikuwa thamani ndogo ya shiling ilisababisha dollarization. Lakini mara dollarization ilipoota mizizi ika-take over na kudidimiza shilling. Au sio?
Kama uelewo wangu hapo juu ni sahihi, basi inamaana kwamba kama benki kuu wakiweza kudhibiti ishu ya dollarization, basi wanaweza kuikoa shilling kwa kiasi fulani. Si ndio?
Kwa sababu, demand ya dollar imeongozeka maradufu mara baada ya baadhi ya wafanya biashara kujiingiza kwenye dollarization system. Hivyo basi, ili kuweza kuinua thamana ya Tshs angalau kiduchu, itabidi dollarization idhibitiwe. Matokeo safari za kwenda kubadilisha hela zitapungua, na mwishowe Bureau De Change watapunguza bei za Dollar.
Kama nimekuelewa vizuri - kwa hiyo mwanzo ilikuwa thamani ndogo ya shiling ilisababisha dollarization. Lakini mara dollarization ilipoota mizizi ika-take over na kudidimiza shilling. Au sio?
Kama uelewo wangu hapo juu ni sahihi, basi inamaana kwamba kama benki kuu wakiweza kudhibiti ishu ya dollarization, basi wanaweza kuikoa shilling kwa kiasi fulani. Si ndio?
Kwa sababu, demand ya dollar imeongozeka maradufu mara baada ya baadhi ya wafanya biashara kujiingiza kwenye dollarization system. Hivyo basi, ili kuweza kuinua thamana ya Tshs angalau kiduchu, itabidi dollarization idhibitiwe. Matokeo safari za kwenda kubadilisha hela zitapungua, na mwishowe Bureau De Change watapunguza bei za Dollar.