Hahaha wanasema tatizo ni barabara mbovu, serikali wakijenga barabara wenye viwanja watakuja kujenga.
Serikali waliuza ardhi na kuchukua pesa, miundombinu wakawaachia wananchi ndio wajenge. Hilo ndio tatizo kubwa katika nchi hii, bila barabara, maji na umeme wengi wanashindwa kuviendeleza viwanja vyao.
Wito kwa serikali, wanapouza viwanja watenge pesa kuchonga barabara, wahimize Tanesco kuleta umeme, pia dawasco walete maji. Maji na umeme vinalipiwa na watumiaji, hakuna atakayetumia bure sioni kwanini serikali haioni ni muhimu kuleta huduma hizo bunju B.
Serikali eti imeng'ang'ana kupeleka umeme vijijini wakati mijini maeneo mengibasi, hayana umeme na maji. Hata viwanda vya ice cream tunashindwa kujenga. Wakumbushe lukuvi na mabula wakija bunju B na mabwepanande waje na wahusika wa dawasco na Tanesco, wakileta maji na umeme pia watengeneze barabara nakuhakikishia mapori na hao nyoka watahamia msitu wa pande.