BUNGENI: Waliobomolewa nyumba zao mabondeni kutolipwa fidia

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Hayo yameelezwa Bungeni na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mbunge wa Wingwi Kisiwani Zanzibar Juma Kombo Hamad ambaye ametaka kujua ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi ambao wamevunjiwa nyumba zao bila ya Serikali kuwalipa kwani wakati wakijenga Serikali iliwaona na kukaa kimnya.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Mabula amesema kwamba kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 inaweka bayana sehemu ambazo wananchi hawatakiwi kujenga ikiwemo maeneo oevu, mabondeni, na vyanzo vya maji ambapo mwananchi akitaka kujenga ni lazima ajenge umbali wa mita 60 maeneo hayo.

Bi. Mabula ameongeza kuwa kutokana na wananchi kukiuka maagizo hayo serikali haitawalipa fidia hivyo ni wajibu wa wananchi kufuata sheria za nchi ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.

Aidha Bi. Mabula amezitaka halmashauri kote nchini kuwa makini katika kusimamia sheria kwani imebainika kwamba nyumba nyingi huwekwa X na halmashauri lakini ufuatiliaji unakuwa haupo ndiyo maana matatizo hayo yamekuwa yakijirudia.
 
Back
Top Bottom