Bungeni: Naunga mkono bajeti asilimia 100, lakini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni: Naunga mkono bajeti asilimia 100, lakini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 4, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,948
  Likes Received: 37,474
  Trophy Points: 280
  Habari wakuu,

  Hivi kweli kuna bajeti ya wizara yoyote hapa nchini inayostahili kuungwa mkono kwa asilimia mia moja?

  Binafsi huwa nashangwaza sana na wabunge wanaosimama na kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja wakati bajeti hizo zimejaa mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutengewa fedha kidogo na ahadi ambazo hazikutekelezwa katika bajeti zilizopita.

  Kwa mfano, bajeti ya wizara ya kilimo ilikuwa na mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutotekeleza ahadi za upelekaji wa chakula cha njaa katika maeneo mbali mbali nchini,matatizo ya pembejeo,bei zisizoridhisha kwa mazao ya kilimo na madudu mengine mengi tu.Pia tukumbuke bajeti ya wizara ya kilimo inayopigiwa chapuo na serikali imetengewa asilimia kumi tu ya bajeti nzima ya serikali!

  Hata hivyo,utashanga kusikia baadhi ya wabunge wakisimama na kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja!Mimi nasema wabunge wa aina hii ni wasaliti,wabinafsi na ni wanafiki wakubwa na wasiopaswa kuchaguliwa tena!Ukiwachunguza kwa makini utagungua kuwa wengi wao wanajipendekeza tu kwa serikali kwa nia ya kupata ama uwaziri au kupata nafasi zingine za uteuzi!

  Ukweli ni kwamba,hata kama kuna utekelezaji umefanywa na serikali katika bajeti husika, hakuna jimbo ambalo limetekelezewa kila kitu kwa asilimia mia moja na hivyo kumfanya mbunge husika kustahili kusimama na kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

  Hivi kweli inaiingia akilini kumsika mbunge mwenzako analalamika kuwa jimboni kwake watu wanakufaa njaa kutokana na serikali kutotekeleza ahadi zake za kupeleka chakula alafu mbunge anaefuata anasimama na kusema naunga hoja mkono asilimia mia moja!Hivi kwanini usimsaidie mbunge mwenzako kuibana serikali itekeleze ahadi zake badala ya kujipendekeza?Hivi kweli sisi ni taifa moja au ni unafiki tu wa kauli za wabunge ndani ya bunge?

  Wabunge wanaounga hoja mkono kwa asilimia mia moja hawawakilishi wanaanchi wao bali ni wasaliti na dawa yao ni kuwapiga chini 2015.Hatupingi serikali kupongezwa ila sio kwa asilimia hiyo mia moja wakati watu wanakufa njaa na hakuna pembejeo na mambo mengine mengi tu.

  Wabunge timizeni wajibu wenu na muache kuleta siasa katika maisha ya watu.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2013
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Nimekuelewa asilimia mia umenena mkuu,magamba safari hii lazima Yapate moto.,wachumia tumbo wa Magamba kama kina Ole Sendeka ndo wanatabia iyo.
   
 3. mbwa mwizi

  mbwa mwizi Member

  #3
  Apr 23, 2013
  Joined: Apr 23, 2013
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hukumu yao imekalibia sana 2015.
   
 4. K

  KWESHELA Member

  #4
  Apr 24, 2013
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni bora wabunge wa CCM wakae nyumbani na kutoa maoni kwa njia ya simu kwa kuwa hakuna jipya wanalofanya ktk kuboresha bajeti zaidi ya kuunga asilimia mia.
   
 5. N

  Ngoso JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2013
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mbunge yeyote anayesimama kuchangia bajet maana yake kaona kuna mapungufu swala la kusema anaunga mkono asilimia mia ni mazoea ya unafiki. Asilimia mia maanayake wameisoma wakaitafakari na kuikubali kama ilivyo bila kuongeza wala kuhoji.
   
 6. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2013
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,872
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kuliona ilo mkuu. Hakika huwa inaniudhi sana na zaidi mbunge anapochangia na kutoa kinagaubaga mapungufu ya mtoa hoja alafu mwishoni akaunga mkono hoja% 100 (tena wengine usema zaidi ya mia).

  Nilisikiliza hoja za mh Mkono na nikapenda uwasilishaji wake wa hoja. Wakati wote anamwambia kwanini aunge mkono hoja kama kuna matatizo haya na yale baada ya miaka 12 akiongelea tatizo iloilo!.

  Nafikiri wakati ni huu wa kuelimisha umma wa watzn juu ya uraghai na unafiki wa wabunge wa ccm (exl mh mkono) at least katk hili.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Yaani kabisa
  Ila hii inafaa jukwaa la chit chat zaidi
   
 8. S

  Skype JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2013
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Kongosho mambo vipi?
  Hujambo lakini?
  Nakuunga mkono mia kwa mia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  lazima utamsikia akisema, Naishauri serikari yangu ya CCM ambayo ni sikivu kwamba....

   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Sijambo za siku?


  Umeona eeh, jukwaa la siasa vikae vya maana
  Uchakachuzi uende kunakostahili

   
 11. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2013
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,440
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Mimi hii mibunge ya ccm ni mburula yote. Mingine ni dr. Prof, darasa la saba lakini itaanza kwa kusema naunga mkono hoja 100% kisha inaanza kutiririka ukosoaji wa hiyo bajeti anayounga mkono asilimia 100 kwa dk 10. Huu ni upuuzi
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2013
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Hiyo kauli hutolewa na wabunge na mawaziri wasio na uelewa wa kutosha na wanafiki tu.
   
 13. j

  jzm-teak JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2014
  Joined: Jun 23, 2013
  Messages: 1,629
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndugu wanaJF n

  Nimekuwa nikifuatilia majadiliano ya bunge letu wakati linaendelea. Nimeona mijadala mbalimbali na hasa inayohitaji kuungwa mkono ili ipitishwe. Nadhani ukiunga kitu mkono na kwa asilimia mia maanake unakubaliana nacho pasipo na shaka.

  Kinacho shangaza kwa hawa waeshimiwa ni kusupprt mjadala asilimia mia moja halafu ataanza kulalamika, mara pesa hazitoshi, mara kijiji changu mmekisahau, malalamiko ni mengi sana!

  mimi napendekeza anayeunga mkono asilimia zote bila kuacha hata moja, aasichangie chochote wenye kuona mpungufu ya mijadala[wasiounga asilimia mia] wapate muda wa kutosha wa kujadili!
   
 14. amakyasya

  amakyasya JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2014
  Joined: Jun 26, 2013
  Messages: 3,463
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Anatakiwa aombewe mapepo yamtoke si akili ya kawaida kuunga mkono hoja 100% wakati kuna matatizo lukuki.
   
 15. msingwa

  msingwa Member

  #15
  Jul 15, 2014
  Joined: Sep 27, 2013
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo mheshimiwa lazima tuelewe kuwa ushabiki ukizidi unapunguza uwezo wa kufikiri, hivyo wabunge wetu wamezidisha ushabiki mpaka wameshindwa kuelewa maana ya asilimia mia moja
   
Loading...