Bungeni: Musukuma na Spika Ndugai waiomba Serikali kuruhusu waganga wa jadi kuruhusiwa kutibu Corona, wadai imani za Kimagharibi ndio kikwazo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma, ameitaka Serikali kuwapa nafasi Waganga wa jadi katika kutumia dawa zao kutibu watu wanaougua Corona.

Amesema akili za Waafrika wengi zimejazwa imani za Magharibi kiasi cha kudharau tiba za asili zilizotumika enzi na enzi.

Aidha, hoja hiyo iliungwa mkono na Spika Job Ndugai, aliyesema yupo Msomi mmoja ameandika dawa zinazoweza kutibu virusi vya corona lakini kutokana na imani za mila za Magharibi hakijapewa kipaumbele.

musukuma 1.jpg
 
Toba! corona wanapelekewa waganga wa jadi?...na hivi wengi ni watu wenye umri mkubwa na hawavaagi barakoa

Nakwambia tutazika Waganga mpaka basi na hivi dawa zao nyingi huwa wanaweka kwenye kapembe halafu wanakupulizia puani daadeeq safari hii Wabunge wa CCM watakosa pa kwenda

Kwa ufupi Msukuma na Ndugai wanaenda kuleta janga lisilo na maana
 
Hizi akili za viongozi wa tanzania ni mbovu sana. Yani wanapoteza posho zetu kujadili maujinga yao eti kwa kua tu rais kajifungia chato akiogopa kolona huku akitaka wengine wachape kazi.....

Tangu lini serikali ikawaomba waganga wa jadi kutibu magonjwa? Mbona hua wanatibu tu wenyewe? Wamechoka kuwaita viongozi wa dini wamekimbilia kwa waganga wa jadi?

Hakuna mbunge anazungumzia na ama kutoa updates NIMR wamefikia wapi na utafiti wao wa dawa au chanjo ya kolona?

Hawa mbwa wanakera sana sana.

TANGU LINI WAGANGA WAKAOMBWA KUTIBU MAGONJWA?
 
Tumefikia hapa kweli??? Ila sishangai hakuna mtu bungeni apo ambaye hafanyi ushirikina.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tiba za asili sio ushirikina tu kama ulivokalili.Mfano kama unaumwa mafua!ukachukua tangawiz asali limao na kitunguu Saum ili kujitibia.Hiyo ni tiba asili tena mzuri sasa ushirikina upo wapi hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ushauri wangu kwa waganga wetu wasikubali kuuwawa kijinga
Shona_witch_doctor_(Zimbabwe)-1.jpg

Hebu fikirieni taifa bila waganga wa jadi...Tanzania inaenda kuwa ya kwanza kupoteza hii tunu tuliotoka nayo kwa wahenga
 
Basi wao wabunge wanze kuzitumia
Naunga mkono hoja mfano kicjocho sionugonjwa was kudungwa misindano ya kizungu na mifonge kibao .Mzizi mmoja tu wa mlenda uliutafuna ukameza mchuzi wake kicjocho kwa heri ya kuonana

Zoko dawa za vidonda za makanisa ya miti kibao ambazo zaweza ponya haraka kuliko za wazungu na bila usumbufu.

Zoko dawa za kusafisha tumbo Kama kwenda chooni shida au una mafuta mengi mwilini Kama mafuta ya nyonyo unakunywa ila ukinywa siku nzima uhamie chooni
 
Back
Top Bottom