Bungeni: Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akwaa adhabu kwa utovu wa nidhamu

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,195
3,331
Mbunge John Mnyika atolewa nje ya Bunge kwa amri ya Spika Job Ndugai na kuamriwa kutohudhuria vikao kwa siku 7 baada ya kutokea malumbano leo.

Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.

Vilevile, Mamlaka ya Bunge kupitia Kamati ya Maadili kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge kutoka nje ukumbi wa Bunge.

Mzozano kati ya Spika na Mnyika





Wabunge wa Upinzani waongea baada ya kutoka nje


=======
UPDATES:


Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ametolewa nje ya Bunge leo Ijumaa kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.


Licha ya adhabu hiyo, amemzuia kutohudhuria vikao vya Bunge kwa siku saba kuanzia leo.

Mnyika ametolewa baada ya mmoja wa wabunge kusema 'Mnyika mwizi' akimhusisha na wizi wa madini, hoja inayochangiwa na wengi kwenye mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini unaoendelea.

Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua kwa mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika akasema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi. Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayaweze kwenda hivyo.

Baada ya majibizano kati yake na Spika, Spika akaamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge na asihudhurie vikao saba vinavyofuata.

Mnyika alikuwa akitoa maelezo baada ya Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde kusema upinzani wa Tanzania ni wa ajabu kwani unatetea wezi wa madini.
 
[HASHTAG]#KutokaBungeni[/HASHTAG] Mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika ametolewa Bungeni na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika. Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.
 
Screenshot_20170602-125040.png

Mwananchi online
 
siasa za bongo kama unga wa ngano yaani unaweza kuwa maandazi mkate chapati bagia au kababu na hata ukipenda visheti pia

Hivi huyu si ndio watizedi walitakiwa kumuombea na akinasibiwa kuwa yuna hekima kumbe ni makinikia tu.

Upinzani wajipange sana hawa masisiemu yaakuwaga na wenge
 
Mbunge John Mnyika atolewa nje ya Bunge kwa amri ya Spika Job Ndugai na kuamriwa kutohudhuria vikao kwa siku 7 baada ya kutokea malumbano leo.

Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.

Vilevile, Mamlaka ya Bunge kupitia Kamati ya Maadili kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge kutoka nje ukumbi wa Bunge
wabunge wamsamehe bure,ndugai ndio aliwafukuza wabunge wa upinzani bungeni wakati wa sheria ya mafuta na gesi,lkn cha ajabu leo hii ndugui naye alionekana bandarani akilalamika kuwa tunaibiwa sana,amerudia makosa yale yale kwenye wizara ile ile
 
Back
Top Bottom