akilimtindi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 421
- 83
Tangu nianze kufatilia siasa za Tanzania ni mara ya kwanza kwa bunge kuongozwa bila ratiba....jana kikao kimeanza spika akahairisha bunge baada ya maswali na majibu ili kutoa nafasi ya kupanga ratiba..
Leo kikao kinaendelea na kuna dalili ya ratiba kutojulikana kinaendelea nini baada ya maswali na majibu. Bila kuficha hii ni dalili mbaya kwa bunge na nchi kwa sasa.
Nchi inakwenda shaghalabagala na hakuna anayestuka, na viongozi wetu wanaona mambo ni sawa tu...na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanadai ni dalili mbaya kwa bunge kukosa ratiba maalumu.
Kuna mambo mengi yanayoonyesha hali ni mbaya, kuna mengine mengi yanakuja muda mfupi unaokuja kwa sababu kwa ufupi serikali imechelewa sana kufanya marekebisho yanayotakiwa ili nchi itulie.