Bunge liwe ni sauti yetu !

Bunge liwe ni sauti yetu !

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
599
Wakuu wana JF,

Heshima kwenu ! Nimetafakari sana juu ya taasisi hii nyeti na moja ya mihimili wenye nguvu sana huu wa dola yaani Bunge na nikaona ipo haja ya kuwashirikisha katika haya mawazo yangu ambayo kimsingi nadhani yana haja ya kusikikaa.

Natamani sana katika Katiba ijayo ambayo nimeshatoa maoni yangu haya kuwa ije na mabadiliko makubwa sana ya kimfumo ya namna ya kujiendesha sisi kama Taifa

• Mawaziri watakaopendekezwa na Mh Rais wajadiliwe na Bunge na hasa kamati husika ya Bunge ili kubaini rekodi zao za kiutendaji katika mahala kwingine walikotoka kabla ya kuapishwa kuwa Mawaziri na Wananchi pia wenye data mbalimbali za wateuliwa hao waweze kuzifikisha mbele ya kamati kwa njia tofauti kama sms , barua pepe na mengineyo !

Hii itatuondolea Mawaziri mizigo na wasio na rekodi zozoote kulipwa mamilioni ya kodi zetu katika utendaji wao wa kazi wa kibabaishaji/ ie Wassira

• Spika wa Bunge na Naibu Spika, hawa wanatakiwa baada ya mapendekezo tu ya majina yao kamati husika kwanza ipokee maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kubaini Mafisadi na watendaji wa bovu katika sekta zingine walizotoka, Mfano Naibu Spika Ndugai zipo taarifa kuwa wakati yupo katika shirika la NORAD la Norway hapa Tanzania alifanya ufisadi mkubwa sana katika utendaji wake wa kazi !

Hakustahili kabisa kuwa Naibu Spika

• Wateuliwa wengine wa Mh Rais ni Makatibu wa Wizara na Wakurugenzi mbalimbali wa mashirika ya Umma. Huku nako ndiko kwenye matatizo halisi ya nchi yetu, Rais kutukanwa na kuonekana ni dhaifu na hawezi kazi yake vizuri kama hao watendaji wake watakuwa watu wa ajabu ajabu wa kuokota okota tu mtaani na kwenye makorido/ viambaza vya mashirika mengine

• Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, kwanza kama ingekuwa ni amri yangu hawa jamaa wasingekuwepo kwenye katiba ya Tanzania wala ya chama chochoote, Nimetoa maoni kuwa hawatakiwi kuwepo maana hata utendaji wao hauna tija kwa Taifa zaidi ya kuwafitinisha na wananchi wa mahala husika na viongozi wengine wa eneo husika ! Mfano Mkurugenzi wa halmashauri angefaa kabisa na yeye na timu yake kufanya kazi zoote kuliko kumuweka huyu mtu hapo ( Mkuu wa Mkoa/ Wilaya ) ni matumizi mabovu ya rasilimali za nchi

• Waziri Mkuu, Siipendi kabisa hii nafasi katika kuendesha serikali maana ipo kisiasa zaidi ! Mkuu gani asiyena uwezo wa kumuwajibisha mtu aliye chini yake ? Rejea kauli ya Pinda juu ya sakata la Jairo !
Nchi iwe na Rais na Makamu wake tu kwishaaaa, hawa watu wakiwa committed wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sanaa,

Makamu wa Rais anafanya kazi ya kutembea na mkasi kwenye koti ili kukata utepe mahala popote atakapoalikwa ! Makamu wa Rais naye pia ajadiliwe Bungeni kabla ya kupewa dhamani kubwa ya kuliongoza Taifa !

Nimetoa maoni yangu kwa njia ya mtandao juu ya Utendaji halisi unaopendeza wa Bunge letu, Bunge lenye meno na Bunge linalotusemea sisi kama Watanzania na wapiga kura ambao tumepelekea sisi kuwapomule ndani ya jengo lile !

Naomba uniunge mkono....kuitendea haki nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba yetu mpyaa...!

The Fixer,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom