Bunge live 'limeanza'!

Mbulula + kiazi
 
kwa hiyo muda wa kazi TV station huzimwa na matangazo huendelea baada ya watu kurudi kazini? Pia yawezekana sisi tu masikini kwa sababu ya kuangalia bunge live? Nani huwa haendi kazini akabaki kuangalia bunge? vitu vingine kama hamjui ni vizuri kuuliza!
 
Tuwe wakweli, hao maskini unaowasema ndio wale wanaofuata drama za bungeni si lolote la maana. Katika awamu hii maskini wanatakiwa wafanye kazi kwa bidii ili wajikwamue kutoka kwenye umaskini wao.
Mmewawezesha?Miaka 50 baada ya Uhuru umaskini unatisha kwa kufungia matangazo ya Bunge wafanye kazi umaskini utawatoka what a joke,tena tubhu kuita watu maskini hili hali awakujitakia kuwa hivyo.
 
Fikiria zaidi mkuu. .bado! Democracy ina gharama zake! !unapoelekea utataka hata mishahara isilipwe tununue madawati
 
Kwaani kuna siku watz waliacha kufanya kazi sababu ya bunge kuwa live mnaogopa wananchi wakiona bunge watawaadhibu mwaka 2020
 
Nguvu zinazo tumika kushawishi bunge lionekane live zingetumika kuwa saidia wakulima kutafuta masoko ya mazao yao ningeona wabunge wetu ni watu wenye hekima na wana fikilia mbali sana lakini hakuna kitu wanacho kifanya.
 
Sioni ubunifu wowote unaofanywa na wabunge katika majimbo yao kuleta maendeleo wakishirikiana na wananchi wao wengine hata kwenda kusalimia jimboni ni matatizo halafu manasema mnawatetea wananchi kwalipi la maana manalolifanya
 
Kwanini isiwe live hili hali nafanya kazi huku napata habari.
 
Wakati wa bunge live, masaa 8 au 9 yanapotea kwa siku. Elimu ndogo tu ya uchumi utajua thamani ya masaa kazi wanayopoteza Watz kwa kukodoa mimacho kuangalia bunge live badala ya kuchapa kazi. Hao Azam na Star Tv waruhusiwe ku-record na warushe usiku. Uangalie masaa hayo yote usiku shauri yako, kesho yake tunataka uchape kazi tu.
 
Hivi akitokea mtu na kushauri bunge lifutwe kukaa kama bunge na kubakia kamati nasi wananchi tusijulishwe chochote kwa kuwa hayo ni garama kubwa, hilo nalo litapata washabiki?
Ndiyo, hasa hasa likiwa lime anzia ccm, mashabiki wapo kibwena hadi wale wa kulazimishwa
 
Kiuchumi na kinadharia "your statement is unjustifiable " mpaka unieleze mbinu za kumwezesha mtu kuchapa kazi.
 
Tunachotaka mtuambie ni sababu gani zilizosabisha serikali ya matingatinga kuzuia bunge kuoneshwa live. Hakuna hata anayethubutu kueleza sababu japo moja tu zaidi ya kutembea na fisi kwenye mikutano ya hadhara.
Kwani ww shambani unabeba tv yako na kulima nayo ! acha uvivu fanya kazi , wanaotetea jambo hili ni wavivu hawana kazi
 
Hivi akitokea mtu na kushauri bunge lifutwe kukaa kama bunge na kubakia kamati nasi wananchi tusijulishwe chochote kwa kuwa hayo ni garama kubwa, hilo nalo litapata washabiki?
Sisi Magufuri anatosha mengine hatuna habari nayo hata kama hatuna bunge sawa tu , watu wanakaa kupiga porojo eti nipoteze muda kuwaangalia , ukiangalia bunge live ndio unaletewa mkate wa kula , acha uvivu hapa kazi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…