Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Jana kwa mara ya kwanza waandishi wa habari walizuiwa kurekodi shughuli za vikao vya Bunge. Hawakuwa na sababu ya kuwepo bungeni. Nikiwaza kwa sauti na kiujinga ujinga tu nashindwa kuelewa.

1. Pamoja na uozo na ubovu na umizigo wa watendaji wa serikali ya JM Kikwete lakini hatukuona hata mara moja rais mcheshi JK akiwaficha watendaji wake nyuma ya pazia.

Serikali ya JPM na wateule wake wamejinabaisha mbele ya ulimwengu kwamba wako makini na wenye kuichukia rushwa na ufisadi. Tangu mapambano ya dhidi ya ufisadi yaanze hapa nchini, huchokonolewa kwanza bungeni. Sasa, hawa wa utawala huu wanachokificha au wanachotaka kukificha ni nini? Kwa nini wanataka mambo yao yatendeke nyuma ya pazia?

2. Imejulishwa kuwa serikali ya JK haikuwa na makusanyo makubwa ya mapato kama hii ya JPM. Pamoja na umasikini wa serikali ya JK haikuinyima fedha TBC. Alitaka muhimili mwingine wa utawala uonwe na uonekane.

Sasa vipi, serikali ya JPM yenye kukusanya mara dufu mapato kuliko ile ya JK ishindwe kuipatia fedha TBC ioneshe moja kwa moja shughuli za vikao vya muhimili huu- Bunge?

Haya, serikali haina fedha. Wapo wenye fedha, Azam TV, StarTV nk basi waruhusuni hao waoneshe! Hamtaki! Kumbe mnachotaka kuficha nini?


3. Imedaiwa kuwa mara kadha serikali imetumia mabavu na mbinu kadha kuudhibiti muhimili huu (Bunge). Pamoja na hayo, JK hakufika pahala akalizima bunge. Imekuwaje awamu hii mnataka kulizima bunge? Nini mnatafuta? Je! Mnataka serikali tu mwonekane, bunge je?

Kwa mwendo huu, wa kukosa kuliona bunge live hakika Kikwete tutakukumbuka. Serikali yako ilikuwa wazi. Ililiacha bunge liiumbue serikali yako iliyojaa mawaziri mizigo.
Ati serikali hii haina mawaziri mizigo ILA haitaki kuumbuliwa hadharani!

HEKO zako Kikwete kukubali kukosolewa na kuikosoa serikali yako hadharani. Hakika katika hili la Uhuru wa Vyombo vya Habari ulijitahidi kuwa muungwana; japo mwishoni ulijikwaa kuja na sharia ya mitandaoni.

UTAKUMBUKWA JK!
 
Hio Bunge tv aliyozungumza Nape jana na waandishi wa habari sijui itatengemaa lini. But still, awamu ya tano inawapa matumaini zaidi watanzania kuliko awamu iliyopita.
 
Yaani kama huu msimamo ndio utakuwa msimamo wa serikali,hii ndio itakuwa serikali ya.........ngoja niachie hapo hapo.
 
Sifa kubwa ya Rais ni kujiamini na kujiamini kwa Rais kunapimwa kwa ujasiri wa kuacha watu kumkosoa na kuvumilia kukosolewa japo alikuwa na nguvu na ushawishi wa kuzuia wakosoaji kusikika na sio uwezo wa kufoka jukwaani na kukunja uso mara kwa mara!
"Tumefikishwa hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete"- John Mnyika

"Kadhia hii ya kuzuia kusikika Bungeni imetufanya tumkumbuke Rais Mstaafu Kikwete"-Mchungaji Msigwa.
 
Ila najua kuna wabunge wataturekodia tu zile sehemu muhimu...tutazipata.
 
Ni bora magufuli dikteta kuliko JK mpanda ndege

Aliyeanza kuchagua vipindi vy akurushwa vya bunge si Magufuli bali ni Kikwete. Magufuli kwa sababu hana uanfiki yeye kaja hadharani basi ndiyo tofauti yao kwa hili.

Ikumbukwe kwamba kurushwa na kutorushwa vipindi vya bunge ilikuja sambamba na ubabe wa sheria ya Mtandao ambayo uliipa serikali mamlka 100% y akuamua kipi kisikike na kipi hapana.

Hili lilianzishwa na kikwete kwenye lengo la kuchakachua uchaguzi na kuwanyima watu taarifa sahihi ama kamili. Sasa hapa serikali inaamua kibabe kipi watu wakipate na kipi wasikijue. Huwezi kumsingizia magufuli kwa hili. Hli ni Msoga special brand. Magufuli karithi kama alivyorishi mnayoyaona ambayo wala sihitajikusayema. Magu yeye ni kwamba alikotoka hawana unafiki wa kiswahli kiasi kwamba kilichoko kichwani kinasomeka usoni, kilichoko moyoni, kinasikika moja kwa moja kutoka mdomoni bila mawimbi.

Afadhali Mtu aliye wazi kuliko mtu mnafiki anayelimaliza taifa kimya kimya huku akicheka kinafiki!
 
dah sijui nisemeje, kutokurushwa kwa bunge kumeniuma lakini, ukiangalia kwa maono ya mbali, uhuru wa habari na demokrasia kwa Africa una hasara pengine kuliko faida, ukiangalia nchi zenye matabaka makubwa yanayopingana ili kuweza kuyatawala yale makundi ni bora ukatawala kwa nguvu na kibabe kuliko kuruhusu demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari
vyombo hivi hutumika kutoa au kufichua taarifa ambazo zinaleta mgongano na kuchochea chuki zaidi katika jamii ambayo ilikuwa haipo stable na yenye watu ambao wanaweza kuwa influenced sana na wanasiasa
tukichukulia mfano wa nchi ambazo hazina demokrasia wala uhuru wa vyombo vya habari lakini kutokuwa na vitu hivi kumesaidia ni kama Rwanda

Rwanda hakuna demokrasia hakuna uhuru wa vyombo vya habari na kuna mtawala mmoja ambaye amebadilisha katiba ili atawale miaka mingine 7 na pia kumekuwa na shutuma nyingi za Kagame kutesa wapinzani wake na wengine kutokomezwa ki mafia,
ukiangalia hapa ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia na lakini ia Rwanda ni nchi ambayo ilikuwa na makabia mawili hasimu ambayo kama uhuru huo wa kujielezea, demokrasia ungekuwepo ungeweza kuamsha tena zile hisia na hata kusababisha machafuko mengine, lakini Rwanda ipo stable na inafanya vizuri

nchi nyingine ni Libya , nchi hii ilikuwa inatawaliwa na Ghadaffi kwa ubabe, alitawala kwa miaka zaidi ya 40 ukiukwaji mkubwa wa demokasia, uhuru wa habari wakosoaji wa serikali pia walikuwa wanateswa kufukuzwa na na kuuwawa
akaondolewa kwa mapinduzi, sasa hivi libya hakuna mtu strong wa kuitawala kibabe tena , bali vikundi vya watu na makabila mbalimbali vikipigana endlessly

Mfano mwingine ni Misri, nchi ya Misri ilikuwa ikitawaliwa na Hosni Mubarak, utawala wake ulikuwa hakuna demokrasia , na upinzani ulikandamizwa sana lakini nchi ilikuwa stable kuliko ilivyo baada ya yeye kuondoka na demokrasia kupanuka

kuna mifano mingi lakini hii inaweza kukuonyesha tu namna uhuru wa habari na demokrasia unavyoweza kuleta hasara kuliko faida kwa nchi za Afrika
 
Kikwete sikumpenda kwa ajili ya chama chake ila alikuwa muwazi aliianika serekali uwozo wote ukajulikana hakuwa mbabe altuacha huru kuzungumza kadili tunavyo weza ametukanwa na kila mwenye kuweza kutukana kakaa kimya kaianika serekali ya ccm lakini kuna marais madicteta hawakutaka kukosolewa uchaguzi ukiisha unasikia yeyote yeyote atakaye leta fyoki asije kulaumu haya Leo tunaogopa hats kuposti maana hata ukichora katuni yenye fanana nae utasikia sheria ya mtando utakamatwa tu tutamkumbuka sana mlisho
 
1954tanu
"Baniani mbaya kia................................."
Nimekumbuka msamiati huu kwa sababu hii hapa; issue ya bunge kutokuwa live au kizungumkuti hicho kilianza wakati gani?

Yaweza kuwa wewe na ndg zako hamumpendi JMP lakini jibu la msamiati hule ndiyo ulikuwa kinga kwa chama kufika hapa, au acha afanye yake hukumu yake kwetu watz ni baada ya kumaliza ungwe yake akiwa robo au nusu muhura!.
 
Mleta hoja una akili timamu kweli au umetumwa? Unamlinganisha na nani? na Magufuli? kwa lipi? hebu toa akili zako za kuambiwa humu!
 
Hio Bunge tv aliyozungumza Nape jana na waandishi wa habari sijui itatengemaa lini. But still, awamu ya tano inawapa matumaini zaidi watanzania kuliko awamu iliyopita.
Hayo ni matumaini ya muda ............. I do not think it will last!!
 
Kikwete anapitia phase ambayo Mkapa alipitia

Mkapa hata kutajwa hakutwa wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Taifa
na Kikwete juzi hata kutajwa hatajwi uzinduzi wa daraja la kigamboni
 
Nadhani ni jambo jema tu kupata yaliyozungumzwa in summary kuliko kuangalia kitu kizima, kwa jamii zetu ambazo bado hatujakua na uwezo wa kumanage matumizi hata ya simu zetu sio vibaya serikali ikitusaidia katika hili, ili tuweke akili zetu katika kuzalisha na tuache wale tuliowachagua wafanye kazi ya kutuwakilishs vyema huko bungeni. Kungangania kutazama bunge live inamaana sisi wananchi hatuna hata imani na wale tuliowachagua kama wanafanya vyema kazi zao, sasa na tuwekeze katika kuchagua wawakilishi sahihi.
 
JK tunamkumbuka kwa yote mema na mabaya yake. Mema tunayaenzi mabaya tunayachukia. Kwa mfano uhuru wa habari huyu Mkwere alitusaidia sana na Mungu ambariki. Ila huyu Magafuli naona ameanza vibaya mapema kabisa
 
Back
Top Bottom