MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kumekua na malamiko mengi sana miongoni mwa jamii kua kuna kasi isiyokukua ya kawaida ya Ujenzi wa miundombinu katika mji wa Chato kuliko miji mingine midogo nchini, miundombinu inayolalamikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato, Ujenzi wa Jengo la TRA linalosemekana kukadiriwa kua na ghorofa mbili au zaidi, Ujenzi wa kituo Cha polisi linalosemekana kukadiriwa kua na ghorofa mbili na zaidi, pia kuna mpangilio wa taa za babarani "Traffic lights" ambazo hata kajika mji wa jirani katoro hakuna.
Kufuta malalamiko haya juu ya serikali ambayo imekua ikipigia kelele suala la rushwa, tuliombe bunge letu endapo mbunge yeyote atapeleka hoja ya kulitaka bunge kumwagiza mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG afanye ukuguzi ili kubaini ukiukwaji wa taratibu za sheria ya manunuzi au laah, je hata utangazwaji wa zabuni ya mkandarasi wa miradi hiyo ulizingatia vigezo.Hilo likifanyika na majibu sahihi yakapatika basi nafikiri mjadala juu ya maneno maneno kwa Rais wetu mpendwa yataisha.Yafanyike kupitia bunge la vikao vijavyo na ikiwezekana hata kamati ya PAAC ifanye hiyo kazi.
Hatukatai kuhusu kuboresha miundombinu ya nyumbani kwa mkuu wetu wa nchi lakini pia ili kuondoa sintofahamu juu ya hilo ni bora haya yakafanyika, hii ndio busara itakayoendana falsafa ya hapa kazi tu.Kunapokua na hofu juu ya kitu flani inapendeza sana ukweli ukajulikana.
Sikumbuki ni lini mzee wetu mtstaafu aliwahi hata kupanga taa za kutosha pale katika mji wetu wa masasi, maana huo mji majengo yake ya TRA na Kituo cha polisi ni nyumba za kawaida tu, hakuna kiwanja cha kimataifa pale masasi labda cha Chopa pamoja na mji huo kua na kasi kubwa ya maendele kulinganisha na wilaya zingine za mikoa ya kusini.
Tukumbuke kua mzee wetu ndiye mwenye mamlaka ya kuamua chochote, Pesa zote za umma ziko chini ya mamlaka yake! Hivyo watu wanaposikia maneno Kama haya unakua ni mshtuko na sintofahamu kwenye jamii! Hivi inawezekanaje Mkuu wetu anayechukia vitendo vya rushwa akamweka ndugu yake kama PS wizara ya fedha? Tutalikwepaje lile neno "CONFLICT OF INTEREST" kwenye jambo kama hili?
Binafsi moyo Wangu bado unasita kuamini haya mpaka pale CAG atakapoamua kukagua na kuuambia umma kinachojiri kile. Je, kuna ukweli wowote? Wanaolalamika wana ushahidi?Mimi na wewe hatumjui, zipo mamlaka husika kushughulikia hayo mambo.
Duniani kote bunge ndio mhimili muhimu sana unaoweza kuamua hatima ya taifa lolote lile, bunge ndio mhimili pekee wenye meno ya kudhibiti mienendo flani ya viongozi wa mataifa hayo. Bunge pekee ndio lenye mamlaka kuunda utawala wa taifa pekee kuliko mhimili wowote duniani kote.