Bunge lipitie upya kanuni zake za kumuadhibu mbunge aliefanya kosa bungeni hii siyo sawa.

mwasamasole

Senior Member
Oct 25, 2015
106
119
Ninacho jua mm mbunge anachaguliwa na wanainchi ili akawawakilishe katika kupeleka matatizo yao bungeni ili yatatuliwe na serikali na mengine anaweza kuyatatua mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa jimboni kwake. Na endapo jimbo halitakua na mbunge ni dhahir kua matatizo ya jimbo hilo hasa yale yanayo igusa serikali moja kwa moja itakua ni ngum kutatuliwa maana hakuna wa kuyasemea bungeni, sasa kama mbunge amekosea unapompa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge anakua anaadhibiwa mbunge au mwanainchi wa jimbo lake? tupeane mawazo.
 
Ndiyo udikteta wenyewe huo Mkuu Kamati hii ni ya Kuwadhibiti Wabunge wa UKAWA na si kamati ya maadili maana kama ingekuwa ni kamati ya maadili mafisadi ndani ya Bunge akina Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengineo wengi wa CCM wangeshaitwa kwenye kamati hii kwa kukiuka maadili ya Bunge na kupokea pesa za rushwa peza za wizi toka kwa fisadi Rugemarila lakini hili halitatokea kamwe. Kama Kamati hii ingekuwa ni ya maadili Wabunge wa CCM ambao wanarusha matusi ya nguoni dhidi ya Wabunge wa UKAWA wangeshaitwa kwenye kamati hii lakini hili nalo halitatokea.
Bunge hili sasa si Bunge Tukufu tena bali ni Bunge haramu ambalo linafanya kila wawezalo ili kwadhibiti Wabunge wa UKAWA ili washindwe kuhoji maovu mbali mbali ndani ya Serikali na pia kuwawakilisha Watanzania katika majimbo mbali mbali nchini ili wawakilishe Bungeni.

Ninacho jua mm mbunge anachaguliwa na wanainchi ili akawawakilishe katika kupeleka matatizo yao bungeni ili yatatuliwe na serikali na mengine anaweza kuyatatua mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa jimboni kwake. Na endapo jimbo halitakua na mbunge ni dhahir kua matatizo ya jimbo hilo hasa yale yanayo igusa serikali moja kwa moja itakua ni ngum kutatuliwa maana hakuna wa kuyasemea bungeni, sasa kama mbunge amekosea unapompa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge anakua anaadhibiwa mbunge au mwanainchi wa jimbo lake? tupeane mawazo.
 
Mimi ningependelea adhabu iwe ya kukatwa sehemu ya mshahara wake kuliko kunyimwa kuhudhuria vikao vya bunge. Bunge litapata fedha kutokana na faini lakini wananchi wataendelea kuwakilishwa vema.
 
Hivi hakuna jinsi ya kuimpeach mbunge? Mbunge asiye na nidhamu hafai kuwakilisha wananchi wenye nidhamu. Nadhani watu mnachanganya nidhamu na unyonge. Kua na nidhamu sio kua mnyonge au kuonewa bali ni kufuata kanuni, sheria na taratibu mlizojiwekea au zilizowekwa.
 
Na hasa unapomuadhibu kwa kutumia kanuni wakati amechaguliwa kwa mujibu wa sharia. Kuweka kanuni ziwe na nguvu kuliko sharia ni kosa baya na ninashauri hekima itumike kurekebisha hili. Linakera.
 
Back
Top Bottom