singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
JASMINE Tiisekwa Bunga ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la 11 akiwakilisha wanawake wa vyuo vikuu, Mwandishi wetu GRACE CHILONGOLA, amefanya mahojiano na mbunge huyo kueleza pamoja na mambo mengine jinsi atakavyoweza kukabiliana na majukumu ya kofia mbili alizonazo.
Raia Mwema: Wewe ni Mkuu wa Wilaya na pia ni mbunge, ilikuaje ukajiingiza kwenye ubunge wakati tayari una majukumu mengine ya kiserikali kama msimamizi wa wilaya?
Jasmine: Naipenda siasa tangu zamani, nilianza kuipenda siasa baada ya kubaini kuwa mwanasiasa ndio mtu anayeweza kuwaletea maendeleo na kuwatetea wananchi hasa wa hali ya chini. Mwanasiasa ni mtu ambaye atailinda na kuiteteta nchi yake kwa sababu ndiye anayetunga sheria anapokuwa bungeni pamoja na kumwakilisha mwananchi na kama Mkuu wa Wilaya natekeleza sheria zilizotungwa nao. Niliona ugandamizaji katika maeneo mbalimbali niliyopitia kabla ya kufika hapa na kila nilipohoji niliambiwa wabunge ndio wametunga sheria za namna hiyo. Nikaona ni vyema nami nikashiriki na kutumia elimu, taaluma na uzoefu wangu katika kuchangia utungaji wa sheria, nipate sehemu ya kuwasemea wananchi hususani wanawake wa vyuo vikuu kama nikiwa mbunge.
Raia Mwema: Mbio za kisiasa ulizianza lini?
Jasmine: Siku moja niliota kuwa nimekuwa mbunge lakini ndoto ile niliipuuzia kwa kutoipa nafasi. Kimsingi mwaka 2002 niligombea ujumbe wa Serikali ya Mtaa pamoja na nafasi ya ujumbe wa Baraza la Wilaya ya Morogoro vijijini na ujumbe wa kamati ya utekelezaji. Mwaka 2008 niliingia kwenye Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), mwaka 2010 niligombea ubunge wa viti maalum Mkoa wa Morogoro ambapo nilishika nafasi ya tano kati ya wagombea 14 waliokuwepo wakati huo. Na hapo ndipo nilipoanza kujulikana kwenye ulingo wa kisiasa. Mwaka 2014 nilipita bila kupigwa kwenye nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimo SUA Kata ya Magadu.
Mwaka jana niliteuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne kuwa mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na ndio nilipobaini kuwa ile ndoto niliyoota kuwa nimekuwa mbunge imeanza kutoa viashiria vya kweli.
Ilipofika Julai mwaka jana nilichukua fomu ya kugombea viti maalum kupitia vyuo vikuu nikipitia ngazi zote zikiwemo za kupitishwa na chama change, CCM kwenye kura za maoni na Halmashuri Kuu ya Taifa (NEC). Baada ya matokeo ya kura za urais kuipa ushindi CCM niliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum anayewakilisha wanawake wa vyuo vikuu
Raia Mwema: Kaulimbiu ya Serikali ya awamu ya tano ni ‘hapa kazi tu’, kama mbunge mpya unawezaje kwenda na kasi hiyo ?
Jasmine: Kila Rais huwa na kaulimbiu inayomwezesha kutekeleza majukumu yake, kwa kuangalia kaulimbiu zilizopita, kaulimbiu ni kama wimbo unaotumika kuikumbusha jamii kutekeleza wajibu wao. Kupitia kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano watendaji wamepunguza kujiamini na kujawa hofu ya utekelezaji wa majukumu wakati kauli hiyo inamaanisha kila mtu katika nafasi yake aliyonayo kama Mtanzania ataifanyia nini nchi yake, hivyo awajibike kwa kutumia muda mwingi wa kazi kuzalisha ili kuleta maendeleo endelevu. Watu wajitume kutimiza majukumu yao na sio kushurutishwa kama ilivyokuwa mitazamo ya wengi. Hata hivyo kaulimbiu hiyo imesaidia na kuleta chachu ya kuwakumbusha watu kuwa wanatakiwa kuwajibikaji na usipofanya hivyo maana yake hufai hivyo upishe watu wengine wenye uwezo wa kwenda na kasi ya ‘hapa kazi tu’ wachukuliwe nafasi hizo. Kila mtu ajitathmini mwenyewe kabla ya kuchukuliwa hatua kwa kuhakikisha anafuata misingi, kanuni na maadili ya kazi na sio ubabaishaji.
Bunge hili la 11 litafaidika na kaulimbiu hii na msimamo wa Rais kuiunga mkono kwa vitendo. Wabunge wengi wanapigania haki za wanyonge kutokana na nchi kuwa na rasilimali nyingi lakini haiendelei kutokana na hujuma mbalimbali zinazofanywa na watendaji kwenye nafasi mbalimbali, rushwa na ufisadi umekuwa mwingi ukiwemo wa EPA na ESCROW kama ulivyoibuliwa bungeni. Majadiliano yatakuwa ya kuipigisha hatua nchi mbele na sio kuirudisha nyuma.
Raia Mwema: Kama mbunge mpya unadhani bunge hili linakabiliwa na changamoto zipi?
Jasmine: Changamoto kubwa ni uzalendo wa kuipenda na kuitetea nchi kupungua kwa kiasi kikubwa, kwa sasa ubinafsi umetawala, kila mtu anasimamia maslahi yake kuliko maslahi ya kitaifa. Hivyo hoja za msingi zitakazotolewa bungeni kwa kuwa tu zimetolewa na chama fulani basi hazitoungwa mkono na kusababisha mpasuko wa kimaslahi ya kisiasa, kila mtu anahitaji kuonekana zaidi kwa wananchi wake kuliko kusema kuwa sasa tunatetea maslahi ya Taifa. Mfano kwenye halmashauri katika kumpata Meya unashukuru Chama kimoja kuwa na watu wengi ila kumpata Meya ni shida, maslahi ya taifa lazima yapewe kipaumbele. Changamoto nyingine ni ya nidhamu, kutoka au kusimama ndani ya Bunge wakati vikao vikiendelea kutasababisha bunge kushindwa kuendeshwa vizuri, maslahi ya nchi lazima yatangulizwe. Bunge la sasa lina mchanganyiko wa uwakilishi wakiwemo vijana, wasomi, wajasiriamali ambao wana uelewa na uwezo wa kutatua masuala kwa mapana yake hivyo wakitanguliza maslahi ya nchi litakuwa na manufaa kwa nchi.
Raia Mwema: Unawezaje kutenga muda wako kuwatumikia wananchi kwa nafasi yako ya Ukuu wa Wilaya pamoja na ubunge?
Jasmine: Nafasi ya Ukuu wa Wilaya inakutaka muda mwingi kuutumia ofisini kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kwamba siku zote wananchi wamekuwa wakijitokeza kuleta malalamiko na kero za aina mbalimbali. Usipokuwepo ofisini kwa muda mrefu, matatizo ya wananchi yatashindwa kutatuliwa na wakati mwingine unaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Kama Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na vikao vya Bunge vinafanyika mjini hapa ni rahisi kwangu kupangilia muda wa kushiriki kwenye vikao vya Bunge pamoja na kuhudumia wananchi. Pia muda wa chakula pamoja na siku za mwisho wa wiki nazitumia kwa kuwepo ofisini kutekeleza majukumu ya wananchi. Teknolojia inakua na kuongezeka mara kwa mara hivyo nitaitumia teknolojia ya mawasiliano kupata taarifa mbalimbali na kuona namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wanawake wa vyuo vikuu na kusoma taarifa mbalimbali.
Raia Mwema: Kama Mbunge unayewakilisha wanawake wa vyuo vikuu katika Bunge la 11, wanawake watarajie jambo gani kubwa kutoka kwako?
Jasmine: Kupigania haki za wanawake wa vyuo vikuu kwa kupigia kelele kuondolewa kwa mfumo dume ili kuwepo na haki sawa pamoja na kuangalia masuala ambayo ni kandamizi yanayomnyima fursa mwanamke ya kupata elimu au ya kufanya kazi vizuri chuoni. Katika vyuo vingi hapa nchini nafasi tatu za juu zote zinaongozwa na wanaume, sasa unajiuliza kulikoni? Kwani hakuna wanawake wenye uwezo wa kushika nafasi hizo, ni lazima wafike mahali waseme kwa kuwa vyuo vinahusisha wanawake na wanaume, basi uongozi uchanganyike ili wanawake nao wapate nafasi ya kutetewa hata kwenye bajeti. Mbali na usawa wa jinsia katika nafasi za uongozi, pia nitaangalia masuala ya mahusiano ya kingono ili mwanafunzi wa kike aweze kufaulu, aondokane na masuala kandamizi wanayofanyiwa watoto wa kike. Wategemee watawakilishwa vizuri kwa sababu nayafahamu masuala mbalimbali ya ukandamizi wa wanawake. Niwatoe hofu wanawake wa vyuo vikuu kwani nafahamu uwakilishwa wangu kwao na matarajio waliyonayo kwangu.
Sehemu ya likizo yangu nitaitumia katika kuvitembelea baadhi ya vyuo vikuu ili kusikiliza changamoto mbalimbali na kuangali vyuo ambavyo havikidhi haja ya wanawake kushindana kwenye soko la ajira ambapo nitaitumia kukutana na wanafunzi wa kike pamoja na wafanyakazi.
Dk.Jasmine alizaliwa Aprili 4, 1962 katika Tarafa ya Mgeta, kijiji cha Nyepenu Wilaya ya Mvomero, ni mama wa watoto watatu. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya na baadae Mbunge wa viti maalum alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, na kwa sasa ni miongoni wa wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge. -