Bunge likinyamaza nchi itaenda harijojo

wopiha

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
246
168
Bunge letu tukufu linatakiwa sasa lichukue nafasi yake ya kuisimamia serikali. Kama litanyamazia vitisho inavyopewa basi itakuwa ni kosa kubwa la kihistoria.

Sisi wananchi tutawalinda kwa kura. Wabunge hasa wa CCM fungukeni muiokoe Tanzania inakoelekea ni shimoni. Kiongozi anavamia kituo cha Redio ninyi mpo kimya, kiongozi ana vyeti feki mpo kimya! Mnataka mpaka aanze kupiga watu barabarani ndiyo mtoe kauli?

CHONDE CHONDE iokoeni TANZANIA.
 
Wameshatia Nanga kuwaondoa ni shughuli kweli kweli kama ni mto ameshavuka mamba ndio wanainua vichwa juu:):):)
 
ameingia kwenye vitabu vya historia mkuu alieingia kituo cha tv na mabunduki ili show irushwe hewani !!Ama kweli Mungu hamfichi mnafiki
 
kilichobakia pale BOT wataambiwa "print more money" (in Idd Amin's voice)
 
Katiba ilileta UKAWA (strongest opposition kwenye historia ya TZ), Uvamizi umeleta umoja kwenye vyombo vya habari..sasa bado one step to go itakaoleta umoja wa wananchi still counting [HASHTAG]#asikimbiemtu[/HASHTAG]
 
Meli imetia nanga maji yamepungua kwenye kina haiwezi kuondoka

Kiburi kimechukua hatamu yake hakiwezi kuondoka kwa kuwa kimejenga mazoea
 
Bunge letu tukufu linatakiwa sasa lichukue nafasi yake ya kuisimamia serikali. Kama litanyamazia vitisho inavyopewa basi itakuwa ni kosa kubwa la kihistoria.

Sisi wananchi tutawalinda kwa kura. Wabunge hasa wa CCM fungukeni muiokoe Tanzania inakoelekea ni shimoni. Kiongozi anavamia kituo cha Redio ninyi mpo kimya, kiongozi ana vyeti feki mpo kimya! Mnataka mpaka aanze kupiga watu barabarani ndiyo mtoe kauli?

CHONDE CHONDE iokoeni TANZANIA.
Umeyaona hayo mawili tu.Yaani nilidhani unaongelea mambo ya muhimu Kama huduma za maji, elimu, afya,umeme, miundo mbinu na huduma nyingine za kiutu Kama ulimchagua Mbunge wako kwa ajili ya kuja kushindana na Rais rudi nyuma kajipange upya manake hapa umepotea njia.
 
Back
Top Bottom