Bunge likikosea likubali na lijisahihishe

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Gazeti la Nipashe ktk toleo lake la jana tarehe 16.04.2016 liliripoti bunge kuufyata kufuatia sakata kati ya kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi.

Taarifa ya gazeti la Nipashe ilitokana na taarifa iliyotolewa na bunge likikanusha kupitia kamati yake ya PAC kwamba iliomba kupatiwa mkataba huo pindi ilipokutana na watendaji wa Jeshi la Polisi tarehe 5.05.2016 na kutilia shaka juu ya utekelezwaji wa mkataba huo.

Kwa mara nyingine tena bunge limekuja kivingine likiwa na taarifa kali inayolishutumu gazeti hilo na kulitaka liombe radhi kwa uzito uleule.

Mimi ni mmoja wa wananchi ambao nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sakata hili la Lugumi tangu pale lilipoibuliwa na kamati ya bunge kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa PAC Hilary Aeshi.

Ni ukweli uliowazi na usiopingwa kupitia vyombo mbali mbali vya habari hususani kuninga vilionyesha Makamu mwenyekiti huyo akilitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba wa lugumi.

Hoja hapa isingekuwa Nipashe ilifanya nini bali kilichotakiwa kufanywa na bunge ni kuueleza umma wa watanzania kwamba kamati ya PAC ilikosea kuomba mkataba kwa mdomo badala ya maandishi au haikuwa na mamlaka ya kushughukikia jambo hilo na si kuvibana vyombo vya habari kwa makosa yaliyofanywa na kiongozi wa kamati.

Tutambuwe kuwa sote tunajenga nyumba moja na linapotokea tatizo suluhisho si kutafuta au kulaumu ulipoangukia bali tutazame tumejikwaa wapi.

Ni matumaini yangu kama mwananchi na kama mpiga kura bunge litaendelea kusimama ktk ukweli hata kama unauma.
 
anatoa Maamuzi utadhani yupo china Mimi nimeona kwa kupitia ITV huyo mwenyekiti wao akisema anawapa siku tatu wawe wamepewa mkataba leo anakuja tena mtu mwingine anatoa notes ya kuombwa msamaha wakati bunge ndio lilidata media na si media ilitoa taharifa isiyokuepo...mimi nilitegemea Bunge lituombe Msamaha kwa kilichotokea na si kukimbilia kutaka lenyewe liombwe msamaha...
 
Back
Top Bottom