Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,722
Wanabodi,
Hii ni Makala Yangu kwenye Gazeti la Nipashe la Leo.
Angalizo:
Hii Mada ni Swali na Alama ya Kuuliza iko wazi na sio Statement!.
Nimeanza hivyo kwasababu mimi mwenzenu niliwahi kuitwa Bungeni Dodoma kwa kutuhumiwa kulidharau Bunge, kufika kule kule Mbunge aliyenishitaki kwa Spika, hakuiona alama ya kuuliza, Spika hakuiona alama ya kuuliza!, Kamati ya Bunge ilipoiona ile alama, kesi iliishia hapo!.
Hivyo ninapohoji jambo lolote kuhusu mihimili, nakumbushia kabisa kuhusu alama ya kuuliza, ili tusije tena tukaanza kuitana Dodoma!.
Swali ni hili...
Je hili Bunge letu Tukufu, ni Bunge Kibri, na Bunge Jeuri?, Linawezaje Kutunga Tena Sheria Batili Iliyoshabatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania?!. Likaamriwa na Mahakama ya Rufaa, tena chini ya Jaji Mkuu mwenyewe, akisaidiwa na Majaji Rufani 6, jumla Majaji Rufani 7 (Full Bench), Bunge Limeamriwa Kuuondoa Ubatili Huo!, Bunge hili kibri na jeuri, limegoma mpaka leo!, Naomba Tujadili Bunge letu hili Tukufu, Linapata Wapi Kiburi Hiki na Jeuri Hii ya Kuidharau Mahakama?!.
Tanzania tumerithi mfumo wa uendeshaji wa nchi, kupitia mfumo wa mihimili mitatu rasmi ya Serikali, Bunge na Mahakama kutoka kwa wakoloni Waingereza.
Kila mhimili una kazi yake, Bunge kazi yake ni kutunga sheria na kuisimamia serikali, Mahakama kazi yake ni kutafasiri sheria zilizotungwa na Bunge, na utoaji haki ndani ya Jamhuri ya Muungano, Serikali kazi yake ni kutekeleza sheria kwa kutekeleza huku za mahakama na maelekezo ya Bunge.
Kinadharia, mihimili hii yote mitatu, inapaswa kuwa sawa (equal), na kila mhimili una nguvu zake na mamlaka yake, (powers) ambazo hazipaswi kuingiliana, (separation of powers), na kila mhimili, uhuru wake, (independence) ambao haupaswi kuingiliwa na mihimili mingine, na mihimili yote mitatu inapaswa kufanya kazi kwa kuheshimiana.
Kwa vile vyombo hivi vyote vitatu, vinaongozwa na watu, binadamu, na binadamu sio wakamilifu, vyombo hivi vyote vitatu, vikapewa jukumu la kila kimoja kuwa kiranja wa mwingine, kupitia kanuni inayoitwa “the doctrine of separation of powers, checks and balances”, mtanisamehe majina ya baadhi ya kanuni hizi ni majina ya kizungu, sijui Kiswahili chake.
Kanuni hiyo ya ukiranja, unaipa hii mihimili, mamlaka ya kuingilia mhimili mwingine, pale unapokiuka mamlaka yake. Mhimili wa Serikali umepewa mamlaka ya udhibiti wa kuuingilia mhimili wa Bunge na Mhimili wa Mahakama usivuke mipaka ya mamlaka yake. Mhimili wa Bunge umepewa mamlaka ya kuudhibiti mhimili wa Mahakama na Mhimili wa serikali usikiuke mamlaka yake, na Mhimili wa Mahakama umepewa mamlaka ya kulidhibiti Bunge na kuidhibiti serikali, inapokiuka mamlaka yake.
Wakuu wa mihimili hii yote mitatu, wakienda kinyume cha majukumu yao, wanaadhibika kwa kuondoshwa madarakani, Ibara ya 46A, Bunge linaweza kumuadhibu rais anapofanya makosa kwa kumuondoa Mkuu wa Mhimili wa Serikali madarakani, Bunge pia kupitia ibara ya 53A, linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na waziri Mkuu akaondolewa madarakani, Bunge pia linaweza kumuondoa Spika madarakani kupitia Ibara ya 87 ya Katiba ya JMT, ya mwaka 1977. Na Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Jaji Mkuu, akifanya makosa, anaweza kuadhibiwa kwa kuondolewa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 110 ya Katiba. Hivyo wakuu wote wa mihimili wasipotimiza wajibu wao, wanaweza kuadhibiwa, kuwajibishwa na kuondolewa madarakani.
Serikali inapofanya makosa ya ukiukaji wa haki za wananchi, inaweza kushitakiwa mahakamani, lakini sio kwa serikali kuwajibishwa, bali kwa serikali kuamriwa na mahakama kutenda haki kwa lazima kupitia amri 6 za kimahakama za certiorari, mandamus, prohibition, (zuio), harbea corpus, quo warranto na procedendo, mtanisamehe amri hizi nyingine zote hazina majina ya Kiswahili wala Kiingereza, bali ni Kilatini.
Lakini Bunge lisipotenda haki, na mahakama isipotenda haki, kwa mujibu wa katiba yetu, bado hakuna utaratibu wowote wa kuishitaki mahakamani popote au kulishitaki Bunge popote!, na ndio maana Bunge letu limekuwa linatunga sheria batili na mahakama inaishia tuu kuzibatilisha, bila Bunge kuwajibishwa!, na sasa Bunge hili, chini ya mwanasheria, nguli, mbobezi na mbobevu, mwalimu wa sheria wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Dr. Tulia Akson, limetitungia tena sheria batili, ambayo ina kipengele batili kinyume cha katiba ambacho kimeisha batilishwa na Mahakama Kuu, Bunge hili linapata wapi kiburi hiki na jeuri hii ya kututungia tena sheria batili?.
Mfano mzuri ni hii Sheria yetu mpya ya Uchaguzi, ni sheria batili!, muswada ulipotoka tuu, tukasema
Hadi Mama tukamweleza Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!
Ubatili wa sheria hii, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu makini wakiwemo wanasheria manguli wabobezi na wabebovu kujadili na mwisho kutunga sheria nyingine batili kama mazuzu!
Ubatili huu nimeuzungumza sana humu
Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii ilyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.
Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
Serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi huo, na Mahakama ya Rufani, ikatoa uamuzi kwa kusema “The Court is not the custodian of the will of the people”, ukimaanisha Mahakama sio mlinzi wa katiba ya wananchi!. Mahakama ya Rufani, ikalirudisha jambo hilo kwa Bunge lenyewe ndio lirekebishe!, na matokeo yake mpaka hivi sasa ninapoandika andika makala hii, sheria batili hiyo imetungwa tena, kipengele hicho batili bado kinatumika kuwanyima Watanzania haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, kwa kuwalazimisha Watanzania kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa. Pia kunawanyima haki Watanzania kugombea uongozi kwa kuwalazimisha lazima kwanza wajiunge na chama cha siasa!.
Kwa vile hakumu ya Mahakama ya Rufaa, ililiamuru Bunge, kuuondoa ubatili huo, swali la kujiuliza ni kwanini Bunge halijatekeleza huku hii ya mahakama?!. Bunge linapata wapi jeuri ya kutotekeleza hukumu halali ya Mahakama Rufaa?!. Jibu ni moja tuu, Bunge halijatekeleza hukumu hii ya Mahakama ya Rufaa, kwa sababu fulani ambayo niliwahi kuitaja, naomba nisiirudie kuisema, nikaliponza bure gazeti hili kuanza kuitana Dodoma.
Naliomba Bunge letu tukufu, chini ya Spika, mwalimu wangu wa kwanza wa kipindi changu cha kwanza somo la sheria, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Dr. Tulia Akson Mwansasu, awatendee haki Watanzania, kwa kutekeleza amri hii ya mahakama na kutuondolea ubatili huu ndani ya katiba yetu, ndani ya sheria zetu.
Mungu Mbariki Dr. Tulia Aweze
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za Mtoa Mada Kuhusu Bunge

Kwa vile Mkuu wa nchi ni rais wa nchi, na mkubwa ni jalala, hivyo likitokea tatizo lolote, analaumiwa mkuu wa nchi, na madudu yote hayo yalitokea kabla Rais Samia hajaingia madarakani, hivyo nimemjengea indemnity Rais Samia asilaumiwe kwa madudu haya Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.Ubatili huu nimeuzungumza hapa
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
- Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?
- Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii ilyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.
Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
- Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi huo, na Mahakama ya Rufani, ikatoa uamuzi kwa kusema “The Court is not the custodian of the will of the people”, ukimaanisha Mahakama sio mlinzi wa katiba ya wananchi!. Mahakama ya Rufani, ikalirudisha jambo hilo kwa Bunge lenyewe ndio lirekebishe!, na matokeo yake mpaka hivi sasa ninapoandika andika makala hii, sheria batili hiyo imetungwa tena, kipengele hicho batili bado kinatumika kuwanyima Watanzania haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, kwa kuwalazimisha Watanzania kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa. Pia kunawanyima haki Watanzania kugombea uongozi kwa kuwalazimisha lazima kwanza wajiunge na chama cha siasa!.
Kwa vile hakumu ya Mahakama ya Rufaa, ililiamuru Bunge, kuuondoa ubatili huo, swali la kujiuliza ni kwanini Bunge halijatekeleza huku hii ya mahakama?!. Bunge linapata wapi jeuri ya kutotekeleza hukumu halali ya Mahakama Rufaa?!. Jibu ni moja tuu, Bunge halijatekeleza hukumu hii ya Mahakama ya Rufaa, kwa sababu fulani ambayo niliwahi kuitaja, naomba nisiirudie kuisema, nikaliponza bure gazeti hili kuanza kuitana Dodoma.
Naliomba Bunge letu tukufu, chini ya Spika, mwalimu wangu wa kwanza wa kipindi changu cha kwanza somo la sheria, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Dr. Tulia Akson Mwansasu, awatendee haki Watanzania, kwa kutekeleza amri hii ya mahakama na kutuondolea ubatili huu ndani ya katiba yetu, ndani ya sheria zetu.
Mungu Mbariki Dr. Tulia Aweze
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za Mtoa Mada Kuhusu Bunge
- Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
- Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?
- Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
- Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?
- Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?