Bunge lakataa kubariki "Division 5"

Tuna aina nyingi za madini,madini hayo ni makristo,malokole,maislam na mengineyo mengi yapatikanayo kila sehemu Tanzania..
 
Hakika sarakasi katika mfumo wa elimu zinazidi kuua elimu ya Tanzania.
 
Nchi hii hata mtawala hajulikani ni nani!hakuna coordination kabisa ktk govt na mihimili mingine
 
Bunge linagombania kuwa na division zero?
Hakuna kitu kinaitwa Division Zero. Hizo ni tungo zenu. Baada ya Division 4 linalofuata ni F. Maana yake Failure (Kushindwa). Sasa wanataka kulemba F iitwe Division 5. Hata hayo madaraja mengine nayo yamepunguzwa alama zake. Hiyo inamsaidia nini mtahiniwa? Kwani tatizo lilikuwa ni ugumu wa mitihani au uwelewa/weledi wa wanafunzi? Kilichokuwa kimefanyika ni wrong prescription for the wrong disease. Kuna hoja zimejengw kuwa hakuna anayetoka shuleni bila kitu chochote hivyo si haki kusema kuwa mtu ameshindwa shule. Kinachopimwa na mitihani ni uelewa na kumbukumbu ya mwanafunzi wa alichofundishwa darasani. Kama unataka kupima umahiri wake wa ku-rap tafuta njia zingine za kufanya hivyo. Mitihani siyo njia sahihi.
 

Something has to be done! nimeiona hii mahala..nimesitika sana!

 
"Mwenyekiti wangu alisema kile hakiwezekani"... sasa hayo ni maamuzi ya kamati au ya mwenyekiti?...
 
Halafu huyu Ngonyani aka Profesa Maji Marefu hakumaliza hata darasa la saba masikini ya Mungu lakini ameonesha upeo hapa kuliko dokta waziri wa elimu na profesa katibu wa wizara.
Kaonyesha upeo au katumwa na kamati kwenda kusema?
 
Very good JK. Mwakani lazima ufaulu utakuwa 100% halafu ufahamu utakuwa -100%.
 
Huyu Mh Ngonyani anachokisema, kinanitia wasiwasi. Ana maana watendaji sasa wanatakiwa kupata kibali kwa Kila kitu cha kiutendaji kutoka Bunge (au Kamati zake) kabla ya kutekeleza kwa sababu bunge lina wataalamu katika Kila eneo? Hii ndiyo kazi ya bunge. Cha ajabu wanakazania mfumo wa alama za ufaulu badala ya kuangalia kiini cha tatizo kwenye mfumo wetu wa elimu!
 
Kimsingi sijawahi ona mpare Pentium One kama huyu Prof(Papaa) Mchome
 
Mwanafunzi anaingia na alama 40, tayar ameshafaulu. Dah, sijui nirudie mtihani!!?? Kweli hii wizara full majanga kisa big result now! Tafadhalin sana boreshen mazingira ya kujifunza na kujifunzia hzo A zitakuja tu.
 
haya ni majanga na aibu kwa serikali ya CCM. ni kama vile serikali nzima imechanganyikiwa haijui inafanya nini
 
Duh! Hili ndio bunge letu

Mkuu hapa tatizo siyo Bunge, tatizo ni uongozi dhaifu wa Wizara ya Elimu chini ya waziri Kawambwa ambaye hata chama chake kimesema YATOSHA. Hivyo. Iwango havifai kabisa na wala huhitaji PHD kujua hilo. Ila Kawambwa, Mulugo,Mchome na Bhalalusesa ni SUMU mbaya sana kwa elimu.
Wabunge wako sahihi viwango vyote havifai tatizo siyo Div 5 pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…