BUNGE LA TANZANIA WAIGE BUNGE LA MAREKANI

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Katika Mkutano uliopita wabunge wa Tanzania walionyesha mshikamano katika kutetea na kusimamia hoja kadhaa bila kujali itikadi za kisiasa. Wengi tulipongeza hatua hii ya kujali zaidi uzalendo. Hata hivyo, hoja hizi zilihusu zaidi maslahi na haki za muhimili wa Bunge.

Wakati Mkutano muhimu wa Bunge la Bajeti ukitarajiwa kuanza hivi karibuni, wananchi tunataka kuona wabunge wakiendelea kuungana kutetea au kupinga hoja kwa kuangalia maslahi kwa wananchi bila kujali itikadi za kisiasa hata kama hoja hizo zinaletwa na Serikali.

Wabunge wetu wajifunze kutoka Bunge la Marekani ambalo juzi wamekataa kupitisha hoja ya Serikali ya Chama cha Republican ya Rais Trump ya kutaka kubadilisha Sera ya Afya ya nchi hiyo iliyoanzishwa na Serikali iliyopita ya Obama. Pamoja na Bunge la Marekani kuwa na wabunge wengi zaidi wa Chama cha Republican, wabunge hawa wameungana na wabunge wachache wa Democrats na kuwezesha muswada huo kukataliwa Bungeni. Wabunge wa Republicans hawakumwogopa Rais anayetokana na chama chao na wakaangalia zaidi maslahi ya wananchi wa Marekani.

Tunawaomba wabunge wa CCM wafuate nyayo za wabunge wa Republicans kuungana na wapinzani kukataa misuada na hoja zisizokuwa na maslahi kwa nchi hata kama misuada au hoja hizo zimeletwa na Serikali.

Mahanga
 
Solidarity for the betterment of our country...nchi yetu ni kubwa ....nchi hii sio ya watu WAWILI ...Mungu hawezi kukubariki kama madaraka uliyopewa unatumia kunyanyasa na kuminya haki za wananchi...watanzania wa jana sio wa leo..tumeamka na tunaelewa hatuwez kuongopewa kwa lolote...mana dalili.ya udikteta ni kuminya any means wananchi kwanza wasielewe haki.zao na kuminya midomo ya wapinzani..na pia elimu kuminywa pia..ndo mana hata mikopo ya wanafunz imekua shida, wengine nmeona wanarudi.nyumbani ..na mambo meng yanayotokea kutisha watu...Mungu anasema msiogope.
Wabunge wote na vyama vyote tuungane..nchi yetu ni kubwa zaidi ya watu WAWILI.
 
Back
Top Bottom