Bunge la Tanzania linairudisha nyuma nchi

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,578
1,984
Nimesikitishwa sana na jinsi uchaguzi wa EALA ulivyoendeshwa kiasi cha kuvikosesha vyama vyanye haki wabunge wa mujibu wa kanuni. Inaeleweka kwamba CHADEMA ndiyo chama kikuu cha wapinzani na kilikuwa na haki ya kupata nafasi 2, lakini wa figisu za wabunge wa CCM wamewanyima hizo nafasi.

Lengo lao ni kuwanyong'onyeza na kuvibeba vyama dhaifu. Bunge letu lenye wabunge wengi wa CCM limekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi hii. Bunge halina maamuzi na linashindwa kuisimamia Serikali.

Ndio maana wabunge hawa waligombezwa na Rais kama watoto wadogo pale Dodoma.
Sasa tunakwenda kwenye Bunge la bajeti, hakuna kitakachofanyika.
 
Mkuu Tanzania haina bunge bali kuna walaji wa pesa za umma tu, tungekuwa na bunge linalojua wajibu wake Magufuli asingekuwa anajipangia tu matumizi ya pesa za bajeti vile anaona yeye inafaa. Bunge la sasa linaongozwa na Magufuli na lenyewe kubaki kuwa rubber stamp tu... Ccm achani ujinga
 
Wote ni wale wale CHADEMA wanapaswa wajipange na kuleta ushawishi kwa wenzao. Jana walikuwa wanataka JK arudi while wao ndio walituaminisha kuwa si kiongozi mzuri.
 
Hivi kwanini Chadema haikupeleka majina mengine pia au wanachama wengine walikataa kuwania ubunge huo?
 
Sioni ulazima wa kuteua wagombea wawili kupitia chadema, ni vyema wangepeleka wagombea 4 ili kutafuta hao wawili
 
Sioni ulazima wa kuteua wagombea wawili kupitia chadema, ni vyema wangepeleka wagombea 4 ili kutafuta hao wawili
Tatizo linakuja Kwa wingi wa kura masisiemu yatachagua watu wasio na uwezo wa kutosha ili kuikomoa Chadema.
 
Issue siyo namba issue hapa nikuikomoa Chadema kwa maslahi ya nani wanajua wa ccm? Kuna haja gani kukaa miezi kadhaa kula posho na baadaye kupitisha budget ambayo haiwezakani kuisimamia! Ni aibu kubwa sana!
 
Wabunge wengi wa ccm wameenda bungeni kwa ajili ya kutafuta mitaji na maisha mazuri usitegemee cha maana kutoka kwa watu wanaotanguliza matumbo wakiacha ustaarabu nyuma
 
Back
Top Bottom