Bunge la Awamu ya 5 limekua puppet wa Serikali

Luse msomba

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
228
159
Nimeanza kuchanganyikiwa, matumaini kama yanaanza kupotea vile. I'm telling you guys. (-1) +(1) = 0. kama bunge litakua ni Toy ya serikali = -1, upande mwingine kuna Magufuli na juhudi zake +1 tutafikaje? hii ni sawa na -1+1. Bunge lijitegemee.

Bunge ni platform ya wanainchi kuisimamia serikali baada ya kuichagua. Tunachokiona sasa ni kwamba hili litakua bunge bovu kabisa kuwahi kutokea Tanzania. Je kwamba tulikosea kwenye uchaguzi? Bunge hawataki tuone wachojadili, Je Mheshimiwa rais nawe unalikubali hili? Mbona mambo mengine umeyaweka hadharani wote tumekufurahia?.

Je serikali haina mkono katika hili? maana Mweshimiwa nape ni waziri wa habari na tumemsikia alichosema.

Bunge hili limepoteza autonomy yake. kwanini? ni kujipendekeza labda? Je Serikali imeingia huku na kulibana?. Malengo na mwelekeo wa bunge hili tulilochagua ni nini? ni kuisimamia au kutetea ya serikali? kilichopo ni geresha tu.

Wanataka kufanyia mambo gizani ili tusijue mabaya yanayoendelea? Pamoja na mazuri yaliyo anza kufanywa kwangu Hii ni kasoro kubwa ya kwanza kwenye utawala wa awamu ya Tano. Mie nachanganyikiwa kwa sababu, Upande mmoja naona dhamira ya dhati ya Rais, Upande mwingine bunge lenye mwelekeo wa maigizo (eti chenge mmoja wa viongozi wa bunge) lililo poteza autonomy na nguvu ya kusimamia serikali.

Mikakati na mwelekeo wa bunge hili ni kuziba maovu yasiwekwe hadharani na kubana demokrasia.Kama bunge halitafanya kazi yake ya kuitetea serikali.. hakuna la maana litakaloendelea. narudia tutabaki kushangilia utumbuaji wa majipu bila achievement yoyote.

Tunataka Bunge lijitegemee. Bunge liisimamie serikali. Ubabaishaji ufike mwisho. Tunataka transparent katika utendaji wa serikali.
 
Back
Top Bottom