Bunge la April 2016 serikali ipeleke mswada wa dharura wa sheria ya kunyonga mafisadi

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Mheshimiwa Magufuli fanya yote ufanyayo lakini chonde chonde kwenye bunge lijalo hakikisha serikali yako inapeleka bungeni tena kwa waraka wa dharura wa kutunga sheria ya kunyonga mafisadi, lakini kama tutaendelea na maigizo ya kuwafunga miaka mitatu kisha wanaachiwa na kupewa gumboot, ovaroli, mifagio na glovu kwenda kukusanya na kuchoma karatasi za Mwananyamala hospitali ni upunguani.

Hiyo nyonga nyonga ndiyo njia pekee itakayoinyoosha hii mijitu yako iliyokuzunguka, yaani mpaka waziri anayesimamia mapolisi yuko kwenye pay roll ya BoT ya kulipwa mshahara bila kufanya kazi? Aibu tupu!

Hivi lile litoto la Korea kaskazini linalonyoa bwenzi linawazidi nini ninyi marais wa Tanzania? Mbona waziri wake wa Ulinzi alisinzia kwenye mkutano wakati toto hilo ambalo ndilo Rais linahutubia akapigwa risasi siku hiyo hiyo kwa kosa tu la kusinzia? Kwani yeye anamwabudu Mungu gani, si huyu huyu wetu?
 
Duh..naona umeandika kwa hisia kali ni jambo jema.
ila ushawahi kujiuliza ikiwa huyo fisadi unaetaka anyongwe ni nduguyo wa karibu alafu ndio mfadhiri wako wa mambo mengi..ni mfano tu

swali ni je? utafurahia unapo mwona katundikwa kwenye ile kamba au ndo utailaani sheria kwakile kinachoenda kufanyika wa nduguyo.
 
Serikali haiwezi kuogopa kutekeleza sheria kama hiyo kwa kuogopa kwamba ndugu wa waharifu hao hawatafurahishwa na adhabu hiyo.
 
Pole sana mkuu, hebu chukua maji unywe kwanza maana ni tiba ya mapema ili kuondoa stress. Sasa, fuatilia vizuri mambo yanavyoenda ndo urudi kuandika kwa kutulia. Asante.
 
Duh..naona umeandika kwa hisia kali ni jambo jema.
ila ushawahi kujiuliza ikiwa huyo fisadi unaetaka anyongwe ni nduguyo wa karibu alafu ndio mfadhiri wako wa mambo mengi..ni mfano tu

swali ni je? utafurahia unapo mwona katundikwa kwenye ile kamba au ndo utailaani sheria kwakile kinachoenda kufanyika wa nduguyo.
kwanza aanze na yule alieuza nyumba za uma alafu wengine wafuatie
 
Hiyo sheria ikipita maana yake ni kuwa ccm itakuwa inazika wanachama wake kila siku, itakuwa ni misiba tu kwa ccm kwa hiyo ccm hawawezi kukubali hiyo sheria ipite
 
Mheshimiwa Magufuli fanya yote ufanyayo lakini chonde chonde kwenye bunge lijalo hakikisha serikali yako inapeleka bungeni tena kwa waraka wa dharura wa kutunga sheria ya kunyonga mafisadi, lakini kama tutaendelea na maigizo ya kuwafunga miaka mitatu kisha wanaachiwa na kupewa gumboot, ovaroli, mifagio na glovu kwenda kukusanya na kuchoma karatasi za Mwananyamala hospitali ni upunguani.

Hiyo nyonga nyonga ndiyo njia pekee itakayoinyoosha hii mijitu yako iliyokuzunguka, yaani mpaka waziri anayesimamia mapolisi yuko kwenye pay roll ya BoT ya kulipwa mshahara bila kufanya kazi? Aibu tupu!

Hivi lile litoto la Korea kaskazini linalonyoa bwenzi linawazidi nini ninyi marais wa Tanzania? Mbona waziri wake wa Ulinzi alisinzia kwenye mkutano wakati toto hilo ambalo ndilo Rais linahutubia akapigwa risasi siku hiyo hiyo kwa kosa tu la kusinzia? Kwani yeye anamwabudu Mungu gani, si huyu huyu wetu?
Hujakurupuka kweli wewe? Angalia asije akanyongwa mzee wako
 
kunyonga sio adhabu nzuri......
adhabu ya kifungo cha maisha ndo solution..................
ila hii haiwez kutokea ndani ya ccm,....wamebinafsisha nchi ccm,....rasilimali zote za nchi ni za watu binafsi,......
katiba chama inasema chama kwanza nchi baadae..............
 
ni sawa na kumwambia mganga ajigange mwenywe
Quando-o-marido-acha-que-%C3%A9-esperto%E2%80%A6-562x330.jpg
 
Back
Top Bottom