Bunge kusitishwa kurushwa live na muelekeo wa siasa za Maahinji ni pigo kwa CDM uchaguz 2020

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Ujio wa katibu mkuu mpya CDM umekuja na mabadiliko makubwa wa namna ya uendeshaji wa siasa za chama hicho tofauti kabisa na style ya siasa iliozoeleka ndani ya chama hiki.
Kwa sasa CDM sio ile ya maandano na harakati nyingi kama ilivyokua hapo awali na hapa ndipo sehemu mahususi CDM inakwenda kuangamia kwani harakati hizi ndio kitu pekee ambacho kilitangaza chama hata kufika hapa kilipo.
Wakati wa Dr Slaa ilikua ni ngumu sana wiki ipite bila taifa kutikisika kupitia media ama mitandao yakijamii ku report jambo lililoibuliwa na CDM eidha kupitia harakati za ndani ya chama ama bunge jambo ambalo kwa sasa halipo.
Kwa sasa inaweza pita muda mrefu sana watanzania wasisikie chochote chakustua akili zao kuhusu chama hiki zaidi ya habari za serikali ya president Magufuli na hii ndio dalili ya kifo cha CDM.Ikumbukwe chama ni kama bidhaa ambayo inahitaji kutangazwa ili image yake isifutike akilini mwa mteja.
Sasa wakati katibu mkuu kaja na style ya kulala usingizi wa pono,kusitishwa kurushwa kwa bunge live kumekua ni msumari wa pili kwa wapinzani kwani Bunge nalo lilikua na mchango mkubwa sana kwenye kuutangaza upinzani.
Leo tunaambiwa bunge limeahirishwa kwa muda baada ya upinzani kuanzisha vurugu ambazo chanzo chake ni kukumbushiwa ufisadi wa lowasa,jambo hili tumeishia kusikia tu hatujaona wakati siasa za aina hii ndani ya bunge ndizo zimechangia kuujenga
upinzani.
Hivyo taaluma ya utabibu ya Mashinji inaweza ikaighalimu CDM kwani kwa hali ilivyo katibu mkuu huyu hana wigo mpana kwenye mambo yasiasa ukilinganishwa na mtangilizi wake Dr Slaa.
 
ingekuwa wewe ni mwana-chadema ningekuelewa,maana haiingii akilini mtu asiye mwanachama kujua weledi wa viongozi wake.tuambie ya lumumba na majipu yaliyojaa humo.
 
Back
Top Bottom