Bunge kurushwa "LIVE" ni sera ya CCM au Serikali?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Uamuzi wa Bunge kuhusu hoja iliohoji wabunge wa wananchi kuhusu kutangazwa mijadala ya bunge " live" unabaki kitendawili kisichokuwa na mteguzi; baada ya wabunge wa CCM kwa wingi wao kubariki hoja ya kulifanya bunge kuwa kama " kibuyu" cha kuteta wanasiasa.

Tujiulize, je, uamuzi huo ni sera ya chama cha CCM za kuwashurutisha wabunge wao kupinga kila hoja inayotoka upinzani ( Mao Tse Tung style ) au ni muongozo kutoka SMT kwenda kwa wabunge wa CCM katika kusherehesha vita vya kubana matumizi?

Kwa dhana zote mbili jibu la moja kwa moja la mwafaka halipo.Ikiwa dhana ya CCM ni kupunguza matumizi kwa nini basi BLW la Zanzibar linalomilikiwa 100% za wawakilishi kutoka CCM matangazo yake yanarushwa " live" wakati serikali ya CCM Zanzibar inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi, na inahitaji sana kubana matumizi? Je, na wao kama wangelikuwa na upinzani kwenye Baraza wangeliungana na ndugu zao CCM bara kupinga kuonyeshwa mahojiano hayo "live"?

Ikiwa dhana hii itasimama, basi tatizo si la kiuchumi ( kubana matumizi) lakini ni hofu ya CCM kuogopa kuzikabili hoja za upinzani mbele ya macho na masikio ya wananchi ( wapiga kura)
 
Back
Top Bottom