G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Hatutaki hoja ya kipuuzi eti ule ni wakati wa kazi! Kusema hivyo ni upuuzi! Ni upuuzi kuwanyima wengi haki ya kuona mambo muhimu kwa mustakabali wa taifa hili kwa hoja ya kipuuzi eti ule ni wakati wa kazi! Kama hoja ni wakati wa kazi basi toeni hoja mitambo yote ya mawasiliano na ya vituo vyote vya radio na tv izimwe ili watu wafanye kazi! Vinginevyo ni upuuzi kusema kuwa watu wajikite kwenye kazi ili eti wasiangalie bunge na wawakilishi wao waliowatuma.
Hatutaki hoja ya kipuuzi eti ni kubana matumizi! Matumizi ya aina gani mnayobana wakati hao TBC1 mshahara tunawalipa sisi? Sasa tusilipe kodi ili mbane hayo matumizi vizuri? Pia hao TBC1 kwanza hawaonyeshi ya maana pale wanapositisha kuonyesha bunge zaidi ya midocumentary ya ajabu ajabu!
Sasa CCM watupe sababu za msingi ni kwa nini wasionyeshe bunge live! Tunashuhudia yale wanayorekodi wabunge wao wanatoa hoja za hovyo hovyo zisizo na mashiko yoyote kwenye jamii.
CCM wanadhani kila kitu ni serikali na ndo maana hadi ubunge wao wameweka rehani serikalini! Sasa serikali ya Magufuli ndiyo inayoliamulia bunge! Huu ni udhihirisho wa utawala usiofuata taratibu kwenye mambo yake na siku sii nyingi kama tutalea haya tutaishia kugharamika kama taifa!
Tuache misingi ichukue taratibu zake!