Bunge kuamua hatima ya tanzania kesho

Bunge kuamua hatima ya tanzania kesho

Joined
Oct 21, 2010
Posts
39
Reaction score
34
Ibara 63(2) na Ibara 4(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 Bunge limepewa mamlaka ya usimamizi wa masuala yote ya umma kwa niaba ya wananchi (Supervisory Authority). Kwa kuzingatia kuwa bunge ndiyo limeanzisha mchakato wa kuchunguza na kufanya maamuzi dhidi ya kashfa ya ukwapuaji wa fedha za umma katika Account ya Tegeta Escrow, kwa hali hiyo basi, Kitendo cha mahakama kuingilia suala lililoanzishwa na Bunge likitumia mamlaka yake ya usimamizi wa masuala ya umma kwa niaba ya Wananchi, ni ukiukwaji wa Katiba ya nchi na Matumizi mabaya ya madaraka.Na hili halihitaji elimu ya sheria kuyaona haya. Ni matumaini yangu kuwa Bunge letu tukufu halitakubali kupokwa madaraka yake kinyume na Katiba ya nchi. Kesho historia itaandikwa, Bunge kuokoa Taifa au Kuangamiza Taifa.
 
Agreed, maana hawa mapimbi wamekimbilia mahakama baada ya kuona propaganda zote zimekwama
 
tena wafukuzwe tu nasema tena wafukuzwe tumechoka na wezi.
 
Bunge ndicho chombo chenye mamlaka ya kuhoji jambo lolote la umma kwa niaba ya wananchi. Mahakama ni dhahiri imeingilia bunge.
 
Back
Top Bottom