mwekundu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2013
- 22,477
- 21,023
Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) linakutana leo jini Dodoma huku hatma ya Mwenyekiti wa umoja huo, Sadifa Hamisi Juma ikiwa mashakani. Mkutano huo wa baraza ulitanguliwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM kilichokaa jana jioni mjini Dodoma kwenye Ukumbi wa White House ambako ni makao makuu ya CCM.
Sadifa, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge, analalamikiwa kutokana na matatizo mbalimbali ya kiutawala, matumizi mabaya ya fedha na usimamizi mbovu wa mali za chama hicho.
Alipoulizwa juu ya kuwapo kwa vuguvugu la kumng'oa, Sadifa alijibu kwa kifupi tu; "Asante Nashukuru." "Ninaambiwa nimekuwa mtu wa kutukana watu, nimemtukana nani? Asante Nashukuru.,"aliongeza Sadifa hata pale mwandishi alipomuuliza kwa zaidi ya mara tatu aliishia kutoa jibu: "Asante nashukuru."
Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda, alipoulizwa na Mwananchi jana, alisema kuwa hana taarifa za kuwapo mpango wa kumng'oa mwenyekiti wake kama inavyoelezwa.
"Sikiliza, mimi ndiye Mtendaji Mkuu wa UVCCM, ajenda za mkutano, sisi kama sekretarieti tumeshaziandaa na hakuna agenda kama hiyo. Umoja huu unaendeshwa kwa kanuni na taratibu,"alisema Mapunda.
Mapunda aliyechukua mikoba hiyo Agosti mwaka huu, alipoulizwa kuhusu mkutano huo kugharamiwa na CCM makao makuu badala ya Jumuiya yenyewe, alikanusha taarifa zilizozagaa akisema: "Mimi ndiye niliyeitisha mkutano huu, sasa chama kinatoka wapi?"
Mjumbe aanika madudu ya UVCCM
Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Ruvuma, Alex Nchimbi alifafanua hakuna njama za kumtoa ila mambo anayotakiwa kurekebisha ndio yanaweza kumtoa.
Nchimbi alisema kuwa UVCCM inakabiliwa na tatizo la matumizi mabaya ya fedha na kibaya zaidi hesabu za chama hicho hazijakaguliwa kwa muda mrefu.
Alisema jumuiiya hiyo hupata kiasi cha Sh80 milioni kutokana na miradi mbalimbali kama jengo lililoko makao makuu ya UVCCM, lakini fedha hizo zinafujwa.
"Ila utashangaa kaka yaani zile fedha zinavyofujwa. Hadi kwa mwezi jumuiya inabakiwa na Sh8 milioni au wakati mwingine hadi Sh6milioni," aliongeza Nchimbi.
source; Bundi atua tena UVCCM - Siasa - mwananchi.co.tz